// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UTATA MATUKIO MECHI ZA AZAM, MACHO YOTE SIMBA NA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UTATA MATUKIO MECHI ZA AZAM, MACHO YOTE SIMBA NA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 01, 2012

    UTATA MATUKIO MECHI ZA AZAM, MACHO YOTE SIMBA NA YANGA



    Azamu fc
    MWANDISHI WETU
    UTATA wa matukio yaliyoibuka kwenye mechi za Azam katika siku za karibuni pamoja na pambano la watani wa jadi ndilo gumzo kwenye Ligi Kuu Bara ambayo Simba ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

    Kuvunjika kwa mechi ya Mtibwa na Azam Jumatatu wiki hii kulikosababisha mwamuzi kupigwa baada ya kuamuru penalti inayodaiwa kuwa ya utata dhidi ya Mtibwa, kumezidi kuzusha maswali mengi kwa wadau wa soka kwamba kuna mbeleko iliyoandaliwa kuibeba Azam msimu huu.

    Mbeleko hiyo pia inadaiwa 'kuhalalishwa' kutokana na mwamuzi kukataa bao la pili la Mtibwa Sugar pamoja na kutoa kadi nyekundu kwa 'Wakata Miwa' hao wa Turiani katika mechi ambayo hadi inavunjika matokeo yalikuwa 1-1.

    Baadhi ya makocha wamekuwa wakidai kuwa mabao mengi ya Azam ni ya kuotea ingawa waamuzi wamekuwa hawana shaka na mabao hayo kwa mujibu wa utaalamu wao.

    Kuna madai pia kuwa hali hiyo ya malalamiko dhidi ya Azam, inatokana na Yanga kutolewa kwenye nafasi mbili za juu.

    Mechi tatu za Azam ambazo zimelalamikiwa zaidi ni dhidi ya Yanga, Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar.

    Katika mechi dhidi ya Yanga ziliibuka vurugu uwanjani kwa wachezaji wa Yanga kumpiga mwamuzi Israel Nkongo kwa madai kuwa alikuwa anaibeba Azam kwa kutoa kadi za njano na nyekundu kwa Yanga.

    Katika mchezo huo, ambao Azam walishinda mabao 3-1, kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima 'Fabregas' alionyeshwa kadi nyekundu pamoja na Nadir Haroub 'Cannavaro'.

    Cannavaro alionyeshwa kadi hiyo kwa kitendo chake cha kumkimbilia mwamuzi na kudaiwa kutaka kumpiga.

    Katika mechi dhidi ya Polisi mjini Dodoma, wachezaji wa Polisi walimvamia mwamuzi, Martin Sanya, kwenye vyumba vya kubadilishia na kumpiga kwa madai kuwa aliibeba Azam na kuipa bao dakika za lala salama.

    Mchezo wa Jumatatu wiki hii baina ya Azam na Mtibwa kwenye Uwanja wa Chamazi, ulivunjika ukiwa na matokeo ya bao 1-1, baada ya mwamuzi Rashid Msangi kutoa penalti dakika ya 87, ambayo Mtibwa waliigomea kwa madai Azam inabebwa.

    Penalti hiyo ilitolewa baada ya Juma Abdul kudaiwa kunawa mpira.

    Mazingira ya penalti hiyo dakika za lala salama, kukataliwa kwa bao la wazi la Mtibwa lililofungwa na Awadhi Issa na kutolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezaji wao Said Bahanuzi yaliwafanya wachezaji wa Mtibwa pamoja na mashabiki kuamini tuhuma zilizozagaa kwa muda sasa kwamba Azam 'imeandaliwa' kushika moja ya nafasi mbili za juu kwenye ligi.

    Mashabiki wengi wameilinganisha kauli binafsi iliyowahi kutolewa na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba, kwamba Azam itashika nafasi ya pili na mazingira ya sasa kuwa yanaendana na hali ya 'kubebwa' huko.

    Mkurugenzi huyo alinukuliwa na Mwanaspoti toleo la Aprili 3, mwaka huu akisema: "Kwa mtazamo wangu binafsi naitabiria Azam FC kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

    "Ni timu ambayo kwa sasa naweza kusema imejitosheleza katika idara zote kiufundi."
    Tayari Azam imeshapewa ushindi wa mchezo dhidi ya Mtibwa, ambapo mwamuzi Msangi pamoja na wasaidizi wake kwenye mchezo huo - Samuel Mpenzu na Abdallah Uhako wa Arusha - wote wameondolewa kwenye orodha ya Ligi Kuu kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wao.

    Lakini hayo yakiendelea, Simba na Yanga zinakwaana Mei 5 katika mechi ambayo Simba inahitaji sare kutangaza ubingwa endapo Azam itaishinda Kagera na Toto Africa.
    Simba ina pointi 59 ambazo kama ikikubali kufungwa na Yanga ambayo imekamia kutibua, Azam inaweza kuwa bingwa kama itakuwa na mabao mengi ya kufunga kwenye mechi zake za mwisho
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UTATA MATUKIO MECHI ZA AZAM, MACHO YOTE SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top