FAINALI ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL)
iliyoshirikisha timu tisa imemalizika jana (Aprili 23 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro huku tatu zikifuzu kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
msimu wa 2012/2013 utakaonza Agosti mwaka huu.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo amesema kwamba timu hizo ni Polisi Morogoro iliyofikisha pointi
20 ikifuatiwa na Mgambo Shooting ya Tanga (15) na Tanzania Prisons ya Mbeya
iliyomaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14.
Wambura alisema kwamba nyingine zilizofuatia na pointi zao
kwenye mabano ni Polisi Dar es Salaam (13), Mbeya City Council (11), Rhino
Rangers ya Tabora (8), Mlale JKT ya Ruvuma (8), Polisi Tabora (6) na Transit
Camp ya Dar es Salaam (2).
0 comments:
Post a Comment