Henry akiondoka na mpira wake baada ya kutupia tatu nyavuni jana |
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry amefunga hat
trick yake ya kwanza katika Ligi Kuu ya Marekani jana akiiongoza New York Red
Bulls kushinda 5-2 dhidi ya Montreal Impact.
Mabao mengine yalifungwa na Kenny Cooper na Mehdi Ballouchy,
Red Bulls ikishinda mechi ya pili mfululizo nyumbani, baada ya kupoteza mechi
mbili za awali ugenini.
New York imefunga mabao tisa katika mechi za nyumbani, matano
akifunga Henry na kutoa pasi mbili za mabao.
Nao Kelyn Rowe na Chris Tierney walifunga kipindi cha kwanza
na kuiwezesha New England kuifunga Los Angeles 2-1, bao la wapinzani likifungwa
na Saer Sene dakika ya 65.
0 comments:
Post a Comment