Hayati Nur Said Mohamed |
RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou, kwa
niaba ya familia ya wapendea soka Afrika imeelezea mshituko na machungu yake
kufuatia kifo cha rais wa Chama cha Soka Somalia, Mr NUR Said Mohamud, baada ya shambulio la bomu katika Mji Mkuu wa
Somalia leo.
Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Taifa ya Somalia, Aden Haji
Yerberow pia aliuawa katika shambulio hilo.“Ningependa kuelezea machungu yangu makubwana kutoa salamu zangu za rambirambi kwa familia za waliouawa katika janga hili sambamba na Kamati ya Olimpiki na familia ya soka Somalia na watu wa Somalia” alisema M. Hayatou.
“Ni siku nyingine ya kiza kwa soka ya Afrika. Ni janga, kama kwa soka ya Somalia imempoteza kiongozi mkubwa na dira ya maendeleo ya soka ya vijana ambayo amekuwa akijihusisha nayo kikamilifu licha ya mazingira ya changamoto kubwa. ” alisema rais wa CAF.
0 comments:
Post a Comment