Talib Hilal |
BEKI wa zamani wa kati Simba SC, Talib Hilal ameteuliwa kuwa
kocha wa klabu ya Al Ahli ya Dubai ya soka ya ufukweni, ambayo itashiriki
michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Akizungumza na bongostaz.blogspot.com jioni hii kutoka Oman
anakoishi, Talib aliyewahi pia kuwa kocha wa muda wa Simba zaidi ya mara mbili,
alisema anatakiwa kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mashindano hayo, yaitwayo MONDIALITO
2012 yatakayofanyika Jijini Sao Paulo, Brazil kuanzia Mei 16 hadi 22.
Talib aliyewahi kuwa pia kocha wa timu ya taifa ya vijana ya
Oman na kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa ya nchi hiyo, anakumbukwa zaidi Simba
kwa mchango wake ulioiwezesha klabu hiyo kuitoa Zamalek mwaka 2003 katika Ligi
ya Mabingwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment