Suarez |
MSHAMBULIAJI Luis Suarez alifunga
bao dakika ya 82 na kuinusuru Liverpool kuzama kwa kulazimisha sare ya 1-1 na
Aston Villa leo katika Ligi Kuu ya England.
Kiungo wa Australia, Chris Herd aliifungia
Villa bao la kuongoza dakika ya 10.
Liverpool imevuna pointi tisa tu
katika mechi 13 mwaka 2012 na inabaki nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi, wakati
Villa ni ya 15, ikiwa na pointi sita tu kutoka kwenye eneo la hatari la kushuka
daraja.
Katika mechi nyingine, Clint
Dempsey alifunga mabao mawili akiiwezesha Fulham kuichapa Bolton 3-0 kwenye
Uwanja wa Reebok katika mechi ya Ligi Kuu leo.
Mshambuliaji huyo wa Marekani
alifunga bao la kwanza dakika ya 25 kwa shuti la umbali wa mita 30 na linguine dakika
ya 45. Mabao mawili ya Dempsey, yanamfanya afikishe mabao 15 katika Ligi Kuu msimu huu na kuvunja rekodi ya
Louis Saha alipokuwa katika klabu hiyo, alifunga mabao 13 mwaka 2004.
Bao la tatu lilifungwa na Mahamadou
Diarra kipindi cha pili.
Bolton inabaki nafasi ya 16, ikilindwa
na pointi moja tu kuanguka kwenye eneo la hatari. Fulham inabaki nafasi ya 10.
0 comments:
Post a Comment