KLABU ya Tottenham imerejea nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuibwaga mabao 2-0 Blackburn usiku huu na kuzidi kuichimbia kaburi.
Rafael van der Vaart aliifungia bao la kwanza Spurs dakika ya 22 kwa shuti kali baada ya kuuwahi mpira uliopigwa kichwa na Gareth Bale na kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Kyle Walker alifunga bao la pili kwa shuti la umbali wa mita 25 dakika ya 75.
Baada ya kushinda mechi moja katika mechi tisa, Tottenham walijua walijua wanahitaji kushinda baada ya kupitwa na Chelsea walioifunga QPR na timu hiyo ya White Hart Lane imefanya ilichohitajiwa na kuzipikuThe Blues na Newcastle kwa kurejea nafasi ya nne.
Spurs sasa watatumaini kuendeleza wimbi la ushindi ili kumaliza katika nafasi ya tatu, wakijua fika, nafasi ya nne haitakuwa nzuri kiasi cha kutosha kuwawezesha kucheza Ligi ya Mabingwa, kama Chelsea itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Mei 19, mwaka huu mjini Munich.
MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MECHI ZA LEO:
0 comments:
Post a Comment