Boban wa Simba kazini |
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Moro United
lililochezwa jana (Aprili 23 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
limeingiza sh. 28,688,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo amesema kwamba jumla ya watazamaji 7,945 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya Sh. 3,000, Sh. 5,000, Sh. 10,000 na Sh.
15,000.
Alisema watazamaji 6,946 kati ya hao walishuhudia mechi hiyo
kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18
ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,376,135.59 kila klabu
ilipata sh. 4,919,009.32, uwanja sh. 1,454,286.44.
Alisema TFF sh. 1,454,286.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,058,414.58, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) sh. 727,143.22, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 145,428.64 na
asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 1,454,286.44.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa
waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000, mwamuzi
wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 80,000,
gharama ya tiketi sh. 3,000,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme
sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing
Construction) sh. 2,000,000.
Nayo mechi kati ya Villa Squad na African Lyon iliyochezwa
Aprili 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam iliingiza sh.
496,000 ambapo kila klabu ilipata sh. 68,061.70 wakati watazamaji walioshuhudia
mechi hiyo ni 469.
Vilevile mechi kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan
iliyochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh.
9,717,000 kutokana na washabiki 2,562.
0 comments:
Post a Comment