Wachezaji wa Simba SC |
WAWAKILISHI wa Tanzania, kwenye michuano ya Kombe la
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Simba wameingia kambini leo kujiandaa na mchezo
wao kwanza wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan, utakaopigwa
mwishoni mwa wiki hii.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema
leo kwamba timu imeingia kambini katikati ya Jiji, kujiandaa na mchezo huo
wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda.
Hata hivyo, Kaburu alisikitika kwamba wapinzani wao hawajatoa
taarifa rasmi ya kuwasili kwao, ingawa wao wamekwishatuma taarifa za mchezo huo
kwa chama cha soka Sudan.
Alisema wachezaji wao wana morali ya hali ya juu na mchezo
huo na benchi la ufundi limeahidi kushinda mabao mengi zaidi ili kujiweka
katika mazingira mazuri katika mechi yao ya marudio.
“Kikosi kipo vizuri na wachezaji wamepania kushinda mchezo
huo, hata hivyo mchezaji Shomari Kapombe alipata maumivu ya mguu kidogo katika
mchezo wa juzi dhidi ya Moro United na
anaendelea na matibabu kama akiwa vizuri kocha anaweza klumpanga hiyo
jumapili,”aliongeza kaburu.
Aidha, Kaburu alisema waamuzi wa mchezo huo Nhleko Simanga Pritchard, Mbingo Petros
Mzikayifani na Sibandze Thulani, Swaziland na Fakudze Mbongiseni Elliot, pamoja
na Kamishna, Kayijuga Gaspard wa Rwanda
wanatarajiwa kuwasili Ijumaa.
0 comments:
Post a Comment