Kikosi cha Simba |
MAKOCHA wa timu za Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan kesho
(Aprili 28 mwaka huu) watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia
walivyoandaa vikosi vyao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.
Itakuwa ni mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la
Shirikisho la Soka Afrika.
Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho itachezwa Uwanja wa Taifa
kuanzia saa 10 kamili jioni.
Simba imefika hatua hii, baada ya kuitoa ES Setif ya
Algeria, wakati Al Ahly Shandy imeitoa Ferroviario ya Msumbiji.
Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo Sudan na mshindi wa
matokeo ya jumla ataingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment