- Sagna exclusiveBacary reflects on Saturday's goalless draw against Chelsea
Bacary Sagna amesema Arsenal haikuwa katika kiwango chake cha ubora katika mechi dhidi ya Chelsea, lakini amefurahia kucheza mechi tano kati ya saba bila nyavu zao kuguswa
Sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates inawabakiza watoto wa Arsène Wenger nafasi ya tatu, wakiizidi pointi tatu Newcastle ambao wana mchezo mmoja mkononi.
Sagna bado hajiamini kwamba wanaweza kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa na amesema timu yao lazima irejeshe fikra zake kwenye mechi dhidi ya Stoke Jumamosi haraka sana.
“Nafikiri dhidi ya Chelsea tulihangaika kugongeana pasi kama kawaida yetu.Hatukukaa sana na mpra na tulisota kutengeneza nafasi,” alisema Sagna . “Lakini angalau hatukufungwa na tumeendeleza kutoruhusu nyavu zetu kutikiswa, hivyo lazima tuangalie mbele katika mchezo ujao.
“Tunataka kurfuzu Ligi ya Mabingwa na tunataka kumaliza katika nafasi ya tatu. Haitakuwa rahisi, lakini tunataka kufanya hivyo.
“Kila mmoja anataka kufuzu Ligi ya Mabingwa . Tottenham wapo nyuma yetu, Newcastle hawako mbali.”alisema.
0 comments:
Post a Comment