// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAFARI NJEMA SIMBA SC, KAWANG'OENI WAARABU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAFARI NJEMA SIMBA SC, KAWANG'OENI WAARABU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 02, 2012

    SAFARI NJEMA SIMBA SC, KAWANG'OENI WAARABU

    Basi la wachezaji wa Simba
    WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya Afrika, Simba SC wameondoka alfajiri ya leo Dar es Salaam kuelekea Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano, Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya wenyeji ES Setif, wakipitia Algeria.
    Simba imeondoka ikisema ina matumaini makubwa ya kuitoa ES Setif katika mchezo huo utakaofanyika Ijumaa wiki hii.
    Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema wachezaji wapo katika ari nzuri na kwamba wimbo wao ni ushindi. Kamwaga aliwataja viongozi watakaofuatana na timu hiyo kuwa ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo Damian Manembe na Kamwaga.
    Alisema benchi la ufundi watakaokuwepo ni Kocha Mkuu Milovan Cirkovic, Kocha Msaidizi Amatre Richard, kocha wa makipa James Kisaka, daktari wa timu Cosmas Kapinga, Nyagawa na mtunza vifaa Kessy Rajab.
    Aliwataja wachezaji waliopo kwenye msafara ni Juma Kaseja, Ally Mustafa, Nassor Masoud, Shomari Kapombe, Amir Maftaha, Juma Nyoso, Kelvin Yondani, Victor Costa, Obadia Mungusa, Jonas Mkude, Patrick Mafisango, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi, Salum Machaku, Uhuru Suleiman, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Edward Christopher, Derick Walulya na Gervais Kago.
    Naye Kocha Mkuu, Milovan alisema wamejipanga vilivyo na kwamba wataufanyia kazi udhaifu uliojitokezakwenye mchezo wa kwanza na kuwaomba mashabiki wasiwe na wasiwasi na kuwa watarejea na ushindi.
    Simba ilishinda mchezo wa kwanza wiki moja iliyopita mabao 2-0, hivyo sare ya aina yoyote au isipofungwa zaidi ya bao 1-0 itakuwa imesonga mbele.
    Katika mchezo huo, Simba baada ya ushindi wa awali wa 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, inahitaji hata sare au kufungwa si zaidi ya 1-0 ili kusonga mbele. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAFARI NJEMA SIMBA SC, KAWANG'OENI WAARABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top