Rooney na Danny |
MSHAMBULIAJI
wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kwamba mshambuliaji pacha wake, Danny Welbeck atafaa
sana kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa klabu hiyo ya Old Trafford,
baada ya mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyol msimu
huu.
Kijana
huyo wa umri wa miaka 21 amefunga mabao 10 msimu huu wa 2011/12 – ukiwa msimu
wake wa kwanza kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha wakubwa wa
timu hiyo.
Lakini
si mabao hayo aliyofunga yanatukuza uwezo wake, bali ni uchezaji wake kwa
ujumla United unaosaidia kampeni za ubingwa, ambao umevutia mashabiki na
wachezaji wenzake kwa ujumla kikosini.
"Kuna
wawania tuzo wachache [ya Mchezaji Bora wa Msimu]… lakini ningeweza kusema Welbeck,"
alisema Rooney.
"Kucheza
mechi nyingi kwa United katika msimu wake wa kwanza wa kuwa mchezaji wa kikosi
cha kwanza limekuwa jambo zuri. Amekuwa na mchecheto sana, lakini amefanya vizuri
haswa na katufungia mabao fulani muhimu.
"Amepata
nafasi tangu mwanzo wa msimu na ameingia na kucheza vizuri sana na kufunga
mabao machache. Ni mchezaji wa kuvutia na anastahili sifa kwa jinsi anavyocheza
– amecheza mechi nyingi msimu huu."
Rooney
amekuwa mtu wa kwanza kumpa sapoti na ushauri pacha wake huyo katika safu ya ushambuliaji
ya United, ambaye amekuwa akimuelewa na anaendelea vizuri.
"Ndio,
imekuwa nzuri," alisema Wazza, alipoulizwa kuhusu pacha yao. "Anaongeza
nguvu nyingi kwenye timu; anapigana kwa juhudi haswa na wakati wote mabeki
wanakuwa nyuma ya miguu yake, ambayo ni babu kubwa kwangu ambayo inajipa mwanya
wa kuuchukua mpira.
"Wakati
wowote ana mishemishe kwenye boksi, ana kasi na ni vigumu kucheza dhidi yake.
0 comments:
Post a Comment