// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RIHANNA HAJIWEZI KWA BROWN, ASEMA WATU WANAJISUMBUA KUMFUATILIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RIHANNA HAJIWEZI KWA BROWN, ASEMA WATU WANAJISUMBUA KUMFUATILIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, April 04, 2012

    RIHANNA HAJIWEZI KWA BROWN, ASEMA WATU WANAJISUMBUA KUMFUATILIA

    Rihanna
    NI zaidi ya miaka mitatu sasa tangu Chris Brown amtende kitu mbaya girlfriend wake wa wakati huo, Rihanna mwaka 2009 na bado nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ameshindwa kumfuta kwenye maisha yake Brown. Tayari ameshirikiana naye katika nyimbo mbili mpya mwanzoni mwa mwaka huu, ambayo inawaweka mashabiki kwenye mazingira mgumu.
    Hivyo kwa nini Rihanna anashindwa kumkunjia ndita moja kwa moja bwana wake huyo wa zamani?
    Katika toleo la Mei, mwaka huu la jairda la Elle, mwimbaji huyo wa wimbo mkali unaotetemesha, We Found Love amefunguka kiasi cha kutosha kwa nini amerudisha mawasiliano na bwana wake wa kale, pamoja na yote aliyomfanyia.
    "Naheshimu wanayosema watu wengine. Kikubwa ni kwamba kila mtu anafikiria kivyake," Rihanna amesema.
    "Ni vigumu sana kwangu kukubali, lakini napokea. Watu wanaishia kupoteza muda wao bure kwenye mablog au popote, wanahangaika, na yote sawa tu. Siwachukii kwa hilo,” alisema.
    Lakini Rihanna anabakia na msimamo wake juu ya kutomtupa Brown katika maisha yake — na hana mpango wa kuomba msamaha kwa hilo. "Kwa sababu kesho nitaendelea kuwa yule yule,"alisem. "Bado nitaendelea kufanya ninachokitaka."
    Ni kwamba mwimbaji huyo amekubali kwamba amejifunza mengi sana katika kipindi kigumu — na sasa yuko jasiri kwa ajili ya hilo. "Imenipa mtutu," alisema. "Nilikuwa kama, poa, k**a. wanafahamu zaidi kuhusu mimi zaidi ya ninavyotaka wajue. Inakera lakini hiyo ilitokana na uwazi wangu. Huo ulikuwa uhuru wangu, wakati wa kutoa hilo. Nilitaka watu wajue mimi ni nani. Vyovyote walivyolichukulia, vizuri au vibaya, nilitaka wajue ukweli."
    Na wakati akiendelea kubaki kuwa mtu maarufu katika macho ya watu, Rihanna anajihisi huru kuliko alivyokuwa daima kabla.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RIHANNA HAJIWEZI KWA BROWN, ASEMA WATU WANAJISUMBUA KUMFUATILIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top