4/25/12 PREMIER | 8:00 PM EDT | SEMIFINAL: REAL MADRID CF (ESP) V. FC BAYERN MÜNCHEN (GER) |
Pre Match
April 25, 2012 2:45 PM EDT
UWANJA: Santiago Bernabéu — Madrid
REFA: V. Kassai
April 25, 2012 2:45 PM EDT
UWANJA: Santiago Bernabéu — Madrid
REFA: V. Kassai
VIKOSI VYA LEO: |
REAL MADRID
CasillasArbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo Khedira, AlonsoDi Maria, Ozil, Ronaldo Benzema |
BAYERN MUNICH
NeuerLahm, Boateng, Badstuber, Alaba Gustavo, SchweinsteigerRobben, Kroos, Ribery Gomez |
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho ana ruhu tupu katika uteuzi wa kikosi kwani ana jeshi kamili tayari kwa Nusu Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa leo dhidi ya Bayern Munich, huku Ricardo Carvalho akiwa majeruhi pekee anaytiliwa shaka.Gonzalo Higuain na Kaka wanaweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo huo ambao Real lazima washinde , wakati Marcelo anaweza kuchukua nafasi ya Fabio Coentrao katika beki ya kushoto.
Kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes aliwapumzisha nyota wake kadhaa katika ushindi wake wa Jumamosi dhidi ya Werder Bremen na atapanga kikosi cha nguvu akitarajia kuulinda ushindi wajke wa awali wa 2-1.
Kiungo mchezeshaji, Bastian Schweinsteiger anatarajiwa kurejea kwenye nafasi yake katika kikosi cha kwanza, lakini mabeki Daniel Van Buyten na Breno wote bado majeruhi.
JE WAJUA? |
- Real Madrid ina rekodi nzuri kwa asilimia 100 nyumbani kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu na imeshinda mechi 10 kati ya 11 za Ulaya Uwanja wa Santiago Bernabeu.
- Los Blancos wamefungwa mechi mbili tu dhidi ya Bayern Munich nchini Hispania, wameshinda sita na kutoa sare moja. Rekodi yao ya jumla dhidi wageni kutoka Ujerumani ni kushinda mechi 17, sare tatu na kufungwa mbili.
- Real Madrid imeshinda jumla ya mechi 22 kati ya 35 za Ulaya ambazo klabu hiyo ilifungwa katika mechi ya kwanza ugenini.
- Gonzalo Higuain, Xabi Alonso, Sergio Ramos na Fabio Coentrao watakosa mechi moja iwapo na leo watapewa kadi za njano.
- Bayern Munich imeshinda mechi moja tu ya ugenini katika mechi zake nne zilizopita kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini imeshinda mechi 11 kati ya 13 zilizopita kwenye mashindano yote.
- Ushindi wa The Bavarians wa 2-0 dhidi ya Villarreal katika hatua ya makundi Septemba, yalikuwa mafanikio ya kwanza ya timu hiyo kwenye ardhi ya Hispania tangu mwaka 2001. Rekodi yao ya nje na La Liga kushinda mechi tano, sare nne na kufungwa tisa.
- Bayern ilishinda mechi za nyumbani 46 katika michuano ya UEFA na ilifuzu katika matokeo ya jumla kwenye mechi zote, kasoro nane.
- Philipp Lahm, Holger Badstuber, David Alaba, Jerome Boateng, Toni Kroos, Luiz Gustavo na Thomas Muller wakipewa kadi nyingine leo, watakosa fainali.
0 comments:
Post a Comment