Ronaldo aliwakosa APOEL Nicosia, vipi leo Bernabeu? |
REAL Madrid inacheza na Apoel leo katika marudano ya Robo
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Santiago Bernabeu, ila ikae ikijua-
Esteban Solari akifunga tu bao, basi APOEL haipotezi mechi.
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho leo anatarajiwa kufanya
mabadiliko fulani kwenye kikosi chake kilichoifunga Osasuna mwishoni mwa wiki. Ricardo Carvalho na Lassana Diarra wote majeruhi, lakini Jose Callejon amepona kifundo cha mguu anaweza kucheza.
Xabi Alonso amemaliza adhabu, lakini anaweza kubaki kwenye benchi, wakati Nuri Sahin anaweza kuwa mbadala wa Sami Khedira, ambaye alikosa mechi na Osasuna kwa sababu ya kuumwa.
Winga majeruhi Angel Di Maria anatarajiwa kubaki katika benchi tena wakati akiendelea kupota nafuu taratibu ili awe fiti kabisa.
APOEL itawakosa Marcelo Oliveira na Ivan Trickovski ambao ni majeruhi walioumia kwenye mechi ya kwanza Cyprus, pia Gustavo Manduca atakuwepo baada ya kumaliza adhabu yake ya mechi moja.
Savvas Poursaitides na Nektarios Alexandrou wote waliumia kwenye mechi ya kwanza, lakini wawili hao wanatarajiwa kuwa fiti kabla ya kipyenga cha kuanzisha mechi ya leo.
JE WAJUA?
•Real Madrid ina rekodi nzuri msimu huu katika Ligi ya
Mabingwa, ikiwa imeshinda mechi nane kati ya tisa ilizocheza hadi sasa.•Los Blancos imeshinda mechi 26 kati ya 27 za Ulaya na inaongoza katika mechi za mwanzo.
•Ushindin wa Madrid wa 3-0 mjini Nicosia ulikuwa wa 200 katika michuano ya Ulaya, yaani tangu inaitwa Klabu Bingwa hadi sasa Ligi ya Mabingwa.
•APOEL ilimaliza katika nafasi ya tatu kawaida katika Ligi Kuu ya Cyprus kabla ligi hiyo haijagawanywa katika katika makundi matatu kati ya manne. Sasa imeingia kwenye mchuano maalum wa kuwania ubingwa wan chi yao dhidi ya AEL Limassol, Omonia na Anorthosis Famagusta.
•Timu hiyo ya Cyprus imeshinda mechi sita kati ya mechi zao nane zilizopita kwenye mashindano yote.
•Esteban Solari amefunga mabao 55 katika mechi 98 za ligi katika misimu yake miwili ya kuwa na APOEL, ambayo haijawahi kufungwa yeye akifunga bao.
VIKOSI VYA LEO:
REAL MADRID: Casillas, Altintop, Pepe, Varane, Coentrao, Granero,
Sahin, Callejon, Kaka, Ronaldo na Higuain.
APOEL: Chiotis, Poursaitidis, Kaka, Jorge, Boaventura, Morais,
Pinto, Charalambidis, Marcinho, Manduca na Ailton.
0 comments:
Post a Comment