Havelange |
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Joao
Havelange bado yuko vema na anaendelea vizuri na matibabu juu ya madhara
yaliyompata kwenye kifundo cha mguu.
Hospitali ya Samaritano imesema Alhamisi kwamba babu huyo wa
Kibrazil mwenye umri wa miaka 95 yuko chini ya uangalizi na tiba makini na
anaendelea kupata dawa za antibiotics. Amekuwa akipatiwa tiba makini tangu amelazwa Machi 18 kwa tatizo hilo ambalo linamsababishia kudhoofu kwa viungo vyake.
Havelange aliiongoza soka duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998. Alijiuzulu katika Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki mwishoni mwa mwaka jana, kwa sababu za kiafya.
0 comments:
Post a Comment