VIKOSI VYA LEO |
MANCHESTER CITY
HartRichards, Kompany, Lescott, Clichy Y Toure, Barry Silva, Tevez, Nasri Aguero |
MANCHESTER UNITED
De GeaSmalling, Ferdinand, Evans, Evra Valencia, Carrick, Scholes, Nani Rooney, Welbeck |
KLABU ya Manchester City inatarajiwa kumrejesha kikosini Micah Richards aliyekuwa majeruhi, wakati mshambuliaji Mario Balotelli naye pia atakuwapo baada ya kumaliza adhabu yake kutocheza mechi tatu, baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi na Arsenal.
Pamoja na hayo, kulingana na kiwango kizuri cha timu siku za karibuni, kocha Roberto Mancini anagtarajiwa kuendelea kuwatumia Sergio Aguero na Carlos Tevez mbele.
Manchester United, itawakosa wachezaji wachache zaidi ya majeruhi wa muda mrefu wanaojulikana Nemanja Vidic, Darren Fletcher na Anderson. Nani, ambaye aliumia kifundo cha mguu mazoezini na Jonny Evans wote kuna hatihati ya kucheza leo, lakini wanatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya mechi hiyo.
Hata hivyo, baada ya kushuhudia akilazimishwa sare ya 4-4 akitoka kuongoza 4-2dhidi ya Everton mwishoni mwa wiki iliyopita, kocha Sir Alex Ferguson anaweza kuamua kubadilisha kikosi chake cha kwanza. Chris Smalling anapewa nafasi kubwa ya kuanza katika beki ya kulia badala ya Rafael wakati kiungo Ryan Giggs, Tom Cleverley, Ji-sung Park na Ashley Young wote wanatarajiwa kuanza pia.
JE WAJUA? |
- Manchester City ina rekodi nzuri nyumbani msimu huu. Timu hiyo ya Roberto Mancini imeshinda mechi 21 kati ya 22 kwenye Uwanja wa Etihad, ikifunga mabao 51 katika mechi 17.
- Wenyeji tayari waliwafunga wageni wao hao wa leo 6-1 kwenye Uwanja wao wa Old Trafford Oktoba mwaka jana katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu, hicho kikiwa kipigo kikubwa zaidi kwa United katika Ligi Kuu daima.
- Katika ushindi wa 6-1, City walikuwa moto mkali mbele ya lango la wapinzani, kwani licha ya kufunga mabao sita, walipiga mashuti nane ya uhakika yenye kulenga goli.
- Pamoja na hayo, kwenye Uwanja wao ni habari tofauti. City haijawahi kufunga bao kwenye Uwanja wa nyumbani dhidi ya United katika ligi kwa takriban miaka mitano sasa.
- Manchester United tayari imeifunga Manchester City mara mbili msimu huu: 3-2 katika Ngao ya Jamii na 3-2 tena katika Kombe la FA, Uwanja wa Etihad, Januari mwaka huu.
- Katika mechi za Ligi Kuu ambazo timu hizo zimekutana kuna kadi nyekundu sita, na Manchester United wana tano na kadi ya mwisho alipewa Jonny Evans (pichani juu kulia katika mechi iliyopita Uwanja wa Old Trafford.
- Mabingwa watetezi wanaingia kwenye mechi hiyo wakiwa wana moto mkali wa kufunga mabao, kwani wamefunga mabao nane katika mechi zao mbili zilizopita, manne dhidi ya Everton na manne dhidi ya Aston Villa.
- Manchester United ilitwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 80 msimu uliopita na hadi sasa tayari wamekwishakusanya pointi 83 na kama wakishinda mechi zao tatu zilizosalia watafikisha pointi 92
0 comments:
Post a Comment