![]() |
| Messi |
GWIJI wa soka Brazil, Pele amesema
kwamba Neymar ni mwanasoka bora duniani zaidi ya nyota wa Barcelona, Lionel
Messi, na amemtaka nyota huyo wa Argentina kwanza ampiku kinda huyo wa Santos kabla
ya kushindajna naye.
Mwanasoka huyo bora wa dunia
mara tatu, akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika hafla ya Santos, alisema
hasikii aibu kuelezea uwezo mkubwa wa Never kisoka.
Babu huyo wa miaka 71 alisema
kinda hyo yuko juu ya Messi katika orodha ya nyota wake wa soka wa duniani hivi
sdasa.
"Sasa kila mmoja anamzungumzia
Messi, ni nyota. Lakini [kuwa bora daima] kwanza lazima awe bora zaidi ya
Neymar," alisema.
"Kwa sasa Messi ni tu ana
uzoefu zaidi."
Mbrazil huyo pia alipuuzia
kuwepo kwa bifu kati yake na Diego Maradona, akisistiza kwamba hakuna kitu kama
hcho baina yao.
"Nyinyi [Waandishi] wakato
wote mnasema mimi ni mpinzani wa Maradona, lakini si kweli. Sijawahi kuwa
mpinzani wake, na alikuwa kiungo mshambuliaji babu kubwa," alisema gwiji
huyo.



.png)
0 comments:
Post a Comment