// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NIZAR KHALFAN SASA KUTUA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NIZAR KHALFAN SASA KUTUA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 01, 2012

    NIZAR KHALFAN SASA KUTUA YANGA



    Nizar Khalfan
    MICHAEL MOMBURI
    SIMBA imefanya mazungumzo na kuafikiana mambo mengi na kiungo Nizar Khalfan, lakini Yanga imeingilia kati na kumuahidi donge nono mchezaji huyo ambaye hajasaini popote.

    Nizar, ambaye aliwahi kuichezea Mtibwa ya Morogoro, yuko nchini baada ya kuachwa na klabu ya Philadelpha Union ya Marekani, lakini Simba na Yanga zinataka kumsajili ingawa amekiri kwamba kama dili za kucheza nje zikiwa freshi hawezi kukaa sana nchini Tanzania.

    Simba walianza kufanya naye mazungumzo kupitia kwa mwanachama wao maarufu Azim Dewji ambaye alitangaza kwamba kila kitu kiko safi na Nizar ni mchezaji wa Wekundu hao, lakini wajumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga wameripotiwa kufanya naye mazungumzo wiki hii.

    Habari zinasema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Seif Ahmed 'Magari' amemuahidi mchezaji huyo Sh 40 milioni na kuwapiku Simba ambao walikuwa tayari kutoa Sh 30 milioni.

    Ingawa Seif hakupenda kuweka wazi suala hilo jana Ijumaa, lakini Mwenyekiti wake, Salum Rupia amekiri kuwa walishafanya mazungumzo na mchezaji huyo.

    Habari za ndani zinadai kuwa huenda wakamsainisha mkataba mchezaji huyo kwa haraka ili kuizidi kete Simba ambayo imekuwa ikitamba kwa karibu wiki nzima sasa.
    Yanga ina kikao kizito leo Jumamosi cha Kamati ya Utendaji kuamua mambo mbalimbali ya klabu hiyo ikiwa ni pamoja na mwenendo wao kwenye Ligi Kuu Bara wanayomalizia na watani wao Simba.

    Nizar aliiambia Mwanspoti jana Ijumaa; "Nimefanya mazungumzo na timu hizo lakini sijasaini kitu chochote, bado nahitaji muda kwa kuwa kuna mambo mengine ambayo nasubiria pia, kwa hiyo yakiwa safi muda wowote naweza kuondoka, lakini ikiwa vinginevyo nitabaki Tanzania.

    "Timu ambayo nitakubaliana nayo itabidi tuafikiane kwamba muda wowote nikifanikisha mambo yangu naondoka, nitakubali kusaini na kucheza hapa kwa sasa ili niwe fiti kwa kuwa nikikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu nalo ni tatizo, lakini haimaanishi kuwa ndiyo nimepanga kubaki moja kwa moja, kuna mambo yangu naangalia mbali zaidi," alisema mchezaji huyo ambaye Mwanaspoti linajua kuna uwezekano mkubwa akasaini Simba kwa sababu ya michuano ya Kombe la Shirikisho na hali ya sintofahamu inayoendelea Yanga baada ya kuutema ubingwa.

    Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' aliposikia jana Ijumaa kwamba Yanga wanamnyatia mchezaji huyo alicheka na kusisitiza; "Hawamuwezi huyo, sisi tumeshafikia hatua ya mbali sana na kuna watu wamekabidhiwa suala hilo kulimaliza, wala halina tatizo.

    Sasa hivi tunaangalia mechi ya Wasudani kwanza." Simba inacheza na Al Ahly Shandy ya Sudan kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho.

    Kwa ujumla hali ya kifedha ya Yanga si nzuri, ingawa kuna baadhi ya watu ndani ya klabu hiyo wapo tayari kuisaidia katika usajili kama walivyofanya msimu uliopita kwa kumsajili Haruna Niyonzima 'Fabregas'.



    GAZETI LA MWANASPOTI:
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIZAR KHALFAN SASA KUTUA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top