Neymar |
MSHAMBULIAJI wa Santos, Neymar alifunga mabao matatu peke yake, wakati timu yake inashinda 3-1 dhidi ya Sao Paulo katika Nusu Fainali ya Campeonato Paulista.
Kinda huyo wa miaka 20 alifunga penalti babu kubwa kipindi cha kwanza kuipa bao la kuongoza timu yake, hilo likiwa la 13 kwenye michuano hiyo na la 100 kwa klabu yake.
Dogo huyo ambaye hivi karibuni Pele amesema ni mchezaji bora wa dunia baadaye akafunga la pili. Alipokea pasi ya Ganso, akamtoka Paulo Miranda na kukwamisha mpira nyavuni.
Willian Jose aliwafungia bao moja wenyeji, kabla ya Neymar kukamilisha hat-trick yake mwishoni mwa kipindi cha pili.
0 comments:
Post a Comment