SOKA YA BRAZIL...
| |
KLABU ya Bolivar ilikuwa na bahati baada ya kutochukuliwa hatua yoyote licha vurugu walizomfanyia nyota wa Santos, Neymar katika mechi ya kwanza ya hatua 16 Bora ya Libertadores Cup mjini La Paz, katika mchezo ambao walishinda mabao 2-1.
Neymar alikuwa anakwenda kupiga kona dakika ya 78 wakati alipopigwa na kitu kutoka jukwaani kwenye Uwanja wa Hernando Siles katika Mji Mkuu wa Bolivian na kuanguka uwanjani.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, alipopigwa tu alianguka chini, lakini mtangazaji wa Televisheni Fox Sports, alisema refa wa Chile, Enrique Osses aliwaonya Bolivar atasimamisha mechi ikwapo tukio kama hilo litajirudia.
Mabingwa wa Amerika Kusini, Santos walibamizwa kwenye ardhi ya La Paz, ulio mita 3 600 juu, awali wakikfungwa Februari mwaka huu katika mwanzo wa kutetea taji lao.
Pamoja na hayo, waliimarika na kushinda katika kundi lao na kusonga mbele .
"Hawapendi kucheza hapa,"alisema mwanasoka wa kimataifa wa Bolivian, Jhasmany Campos, aliyechaguliwa mchezaji bora wa mechi baada ya kutoa mchango mkubwa kwa mabao yote ya Bolivar.
"Tulijipanga kufunga angalau mabao matatu ili kujiweka vizuri kabla ya mechi ya marudiano Brazil, tulijitahidi lakini hatukuweza kufunga zaidi," aliiambia Fox Sports.
Bolivar ilipata bao la kuongoza baada ya sekunde 90 wakati mpira wa adhabu wa kiungo Campos ulipogonga mwamba na kumgonga kipa Rafael na kujaa nyavuni.
timu hiyo ya Brazil ilipata bao lake dakika ya 35 wakati kipa Marcos Arguello alipochupa kuokoa mpira wa adhabu wa kiungo wa zamani wa Brazil, Elano, lakini mpira ulipogonga mwamba na kumkuta beki wa kulia, Maranhao aliyeukwamisha nyavuni.
Bao la ushindi lilipatikana dakika ya 75 pia kutokana na mpira wa adhabu, baada ya shuti la Campos kumpita kipa Rafael aliyejaribu kuchupa kuokoa.
Arguello alimtengenezea Neymar nafasi ya kufunga bao la kusawazisha, lakini kwa bahati mbaya shuti lake likapaa juu ya lango.
Katika mechi iliyozikutanisha klabu za Brazil pekee, Porto Alegre, wenyeji Internacional walilazimishewa sare ya bila kufungana na Fluminense ya Rio de Janeiro katika mechi ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment