Nesta |
BEKI wa AC Milan, Alessandro Nesta amesema kwamba penalti iliyotolewa
kwa sababu yake usiku wa jana katika Robo Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya dhidi ya Barcelona.
Refa Bjorn Kuipers aliamuru penalti baada ya beki huyo wa
zamani wa kimataifa wa Itali kuwafanyia madhambi wachezaji wa Blaugrana, Carles
Puyol na Sergio Busquets katika eneo la hatari wakati wakisubiri mpira wa kona
kabla ya mapumziko.Milan ilikerwa na uamuzi huo, kutoa adhabu wakati mpira haujachezwa wakati huo, na Nesta amesema kwamba hajui kwa nini ilitolewa ile penalti.
"Nilimsukuma Puyol lakini tu baada ya kuniziba mimi," alisema mshindi huyo wa Kombe la Dunia na kukaririwa na tovuti ya Milan.
Licha ya utata ulioigubika penalty hiyo, ambayo ilikwamishwa kimiani na Lionel Messi na kuitengenezea Barca ushindi wa 2-1 na baadaye 3-1 kwa bao la Iniesta, Nesta amekiri timu bora imefuzu Nusu Fainali.
"Barcelona ni wa nguvu," alisema beki huyo kati. "Kama unawaachia nafasi, wanaanza kucheza kama wanaojua wanaojua. Kuna tofauti kubwa kati yetu, lakini nafikiri kwamba Milan wana nguvu ya uchumi na ufundi wa vipaji kuwakaribia siku moja [Barca] au hii timu itaanza kushuka. "Nafikiri katika mechi hizo mbili tumeonyesha kwamba wanaweza kufungwa. Lakini ni ukweli kwamba wanaye Messi, ambaye ni kama una mchezaji wa ziada na vizuri zaidi kwao ni kwamba wanaye.
Hatukuwa na bahati na hakuna aibu ka kufungwa na timu bora duniani. Nina uhakika kwamba Milan itachukua hatua na baada ya miaka kadhaa watarejea kwenye cheche zao kama tulivyokuwa."
0 comments:
Post a Comment