Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru katikati, Rwejuna kulia na Azda kushoto |
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua kinywaji kipya kiitwacho Smirnoff Ice, ambacho
kitaanza kupatikana rasmi leo katika baa mbalimbali na maduka ya vinywani
nchini.
Mkurugenzi Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru Balozi amesema asubuhi hii kwenye Mkutano na
Waandishi wa Habari Ofisi za SBL, Oysterbay, Dar es Salaam kwamba, kinywaji
huko kinakuka kwa ajili ya vijana zaidi ambao damu ya inachemka.
Mafuru
alisema kwamba kinywaji hicho kitakuwa kinapatikana kwa bei ya Sh. 1800 tu na
amesistiza wauzaji wote wa bidhaa za SBL wahakikishe wanauza kwa bei hiyo.
Kwa
upande wake, Meneja wa vinywaji vikali wa SBL, Emmillian Rwejuna alisema kwamba
kutakuwa na matukuio mfululizo ya kutangaza bia hiyo katika kipindi hiki cha
sikukuu za Pasaka.
Rwejuna
alisema kwamba usiku wa leo watakuwa na promotions ya baa hiyo Mbalamwezi,
Mikocheni, Dar es Salaam.
Alisema kuanzia kesho
wataendelea kwenye baa nyingine, Ambrosia, Mafia Lounge, Savanna Lounge ya JB
Belmont Mjini, Jackie’s Pub, Q Bar, Lukas Pub, Didis Pub, zote zipo Masaki na Samaki
Samaki ya Milimani City na Brajec Bar.
“Katika
keuendeleza ugunduzi wa vodka, tunawaletea vodka ambayo tayari imekwishachanganywa.
Mteja hana sababu ya kutafuta kitu cha kuchanganyia, sababu imekwishanganywa na
limao,”alisema Rwejuna.
Kwa
upande wake, Meneja wa Smirnoff Ice, Azda Amani alisema kwamba mara nyingi vinywaji
vikali vimekuwa vinachukuliwa kama vya wanaume zaidi, lakini sasa Smirnoff Ice
ni kwa ajili ya wanawake pia.
0 comments:
Post a Comment