// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWISHO WA BARCA LEO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWISHO WA BARCA LEO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 24, 2012

    MWISHO WA BARCA LEO?


    CL - Chelsea FC v Barcelona, Carles Puyol and Didier Drogba
    Getty Images
     VIKOSI VYA LEO

    BARCELONA

    Valdes
    Alves, Puyol, Pique, Adriano Busquets, Mascherano Fabregas, Xavi, Iniesta
    Messi
    CHELSEA

    CechIvanovic, Cahill, Terry, Cole
    Mikel
    Ramires, Lampard, Meireles, Mata
    Drogba

    KLABU ya Barcelona inaweza kumrejesha kikosini beki wake Gerard Pique, baada ya kupata vipigo viwili mfululizo, kwanza kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Stamford Bridge, kisha kufungwa na wapinzani wao, Real Madrid katika El Clasico Jumamosi, kipigo ambacho kinaonekana kuwafanya waweke rehani taji lao la Primera Liga.

    Wote Carles Puyol na Javier Mascherano wako hatarini kufungiwa, kama wakipewa tena kadi na leo watakosa fainali itakayopigwa mjini Munich, huku timu yao leo ikihitaji kulipa kisasi cha kufungwa 1-0.

    Pep Guardiola leo atakuwa na kikosi kamili- ni uteuzi wake tu mwenyewe awatiumie akina nani, ingawa majeruhi wa muda mrefu  David Villa, Eric Abidal na Andreu Fontas wataendelea kukosekana.

    Kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo anaweza akapanga kikosi kile kile kilichocheza vizuri kwenye mechi ya kwanza, baada ya kuwapumzisha wengi kati yao kwenye mechi dhidi ya  Arsenal mwishoni mwa wiki.

    Mtu pekee ambaye yuko shakani kuonekana uwanjani leo ni mfungaji wa bao la The  Blues kwenye mechi ya kwanza, Didier Drogba, ambaye aliumia goti kiasi cha kutopangwa mechi dhidi ya Arsenal, wakati beki David Luiz bado hajapona tangu aumie kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham.

    Branislav Ivanovic, Ashley Cole na Ramires wote wana kadi moja moja za njano na wako hatarini kukosa fainali mjini Munich mwezi ujao iwapo watafuzu, iwapo wataongezewa kadi leo.
    Chelsea inahitaji sare yoyote ili kusonga mbele, au hata kufungwa kwa tofauti ya bao moja- yaani 2-1, 3-2, 4-3 na kadhalika- wakati Barca inatakiwa ishinde kwa tofauti ya mabao mawili ili isonge mbele.

     JE WAJUA?
    • Barcelona wakifungwa, hiyo itakuwa mechi ya tatu mfululizo na hii ikiwa mara ya kwanza kwao tangu mwanzoni mwa mwaka 2003, ilipopigwa na Valencia, Celta Vigo na Atletico Madrid.
    • Kama kikosi cha Pep Guardiola kitashindwa kuingia fainali maana yake tajio pekee watakalokuwa wanategemea mwishoni mwa msimu huu ni Kombe la Mfalme, watakalogombea na Athletic Bilbao kwenye fainali.
    • Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi (pichani kulia) sasa hivi anajivunia rekoid yake ya kufunga mabao 63 msimu huu, ingawa ameshindwa kutikisa nyavu katika mechi mbili zilizopita.
    • Timu hiyo ya Nou Camp haijafungwa katika mechi saba za Hispania, ingawa tatu za mwisho ziliisha kwa sare.
    • Chelsea imefungwqa mechi moja tu katika mechi zake 14 zilizopita, tena wakifungwa na  Manchester City.
    • Timu hiyo ya Stamford Bridge kwa sasa ipo kwenye nafasi mbaya katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, yaani inaweza kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa mwakani, kwani inashuka nafasi ya sita, ikizidiwa pointi nne na  Newcastle.
    • Wachezaji wakongwe bado wanaonekana kuibeba kwa mabao Chelsea, huku Frank Lampard hivi sasa akiongoza kwa mabao yake 16 msimu huu, wakati Didier Drogba ana 11.
    • Kocha wa Blues, Roberto Di Matteo atashuka Camp Nou akiwa na kumbukumbu mbaya, wakati alipokwendea huko mara ya mwisho kama mchezaji wa timu yake anayoifundisha hivi sasa, walipofungwa mabao 5-1 na kutolewa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWISHO WA BARCA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top