Minziro kulia akiwanoa wachezaji wa Yanga |
KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya Yanga, Fred Minziro (pichani kushoto) amesema ushindi mnono wa mabao 4-1 iliyoupata timu yake juzi dhidi ya JKT
Oljoro ni maandalizi tosha kwa ajili ya pambano lao na Simba.
Minziro alisema wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wako
tayari kwa pambano hilo na kwamba Simba isitarajie mteremko katika mchezo huo
hata kama Yanga imekosa nafasi mbili za juu.
‘’Naenda kupambana na Simba kulinda heshima yangu binafsi na
ya Wanayanga, hivyo Simba wasitarajie kupata ubingwa wao kwa kutufunga hilo
halitakubalika kamwe, ‘’alisema.
Aliwaomba mashabiki wa Yanga watulie na kwamba kushindwa
kutwaa ubingwa mwaka huu itakuwa kichocheo cha kutwaa ubingwa msimu ujao.
Alisema kuanza kuoneshana vidole kwa nini Yanga imepoteza
ubingwa si jambo mwafaka na kwamba kinachotakiwa ni viongozi wa Yanga kusubiri
taarifa ya benchi la ufundi ili waweze kuifanyia kazi.
‘’Hakuna mwana-Yanga mwenye uchungu na timu halafu adiriki
kuihujumu na kama kuna mtu wa namna hiyo huyo hafai na hawezi kuwa Yanga wa
kweli kwani anaweza kuwa mamluki,’’ alisema.
0 comments:
Post a Comment