Soka | Hispania
|
NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amesema jana kwamba alijisikia machungu sana kukutana na vyombo vya habari katika mkutano wa kumuaga Pep Guardiola.
"Nataka kumshukuru Pep kwa moyo wangu wote kwa kila kitu alichonipa katika soka yangu na binafsi,"alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 katika ukurasa wake wa Facebook."Kwa sababu ya machungu, nafikiri sikujisikia kuwapo kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kumuaga Pep na kuamua kukaa mbali na mkutano huo, kwa sababu nilijua wataangalia machungu ya wachezaji kwenye sura zao.
Zaidi ya mashabiki 10,000 waligonga kitupe cha 'Like' kuonyesha kuunga mkono maneno ya Messi na wengine 10 000 wamechangia, wengi wao wakimuunga mkono.
0 comments:
Post a Comment