Messi |
MWANASOKA bora wa dunia, Lionel
Messi wa Barcelona usiku huu amefunga mabao mawili dhidi ya Real Zaragoza
katika La Liga na kufikisha mabao 60 msimu wa 2011-12 katika mashindano yote.
Kijana huyo wa umri wa miaka 24,
aliwafungia bao la kwanza mabingwa hao watetezi wa La Liga na Champions League dakika
ya 39 dhidi ya timu hiyo ya Aragonese, ambayo ilitangulia kupata bao kupitia
kwa Carlos Aranda.
Messi alifunga kutoka umbali wa
mita 15 baada ya kupokea mpira kutoka kwa Alexis Sanchez na kuifanya Barca iongoze
2-1, dakika tatu tangu Carles Puyol asawazishe.
Bao la pili lilitokana na mkwaju
wa penalti, zikiwa zimesalia dakika tano na kuifanya Barca iwe mbele kwa 3-1.
Bao hilo la 60 la Muargentina
huyo, linamfanya abakishe mabao sabatu kufikia rekodi ya Gerd Muller mchezaji
anayeongoza kufunga mabao kwa msimu mmoja Ulaya.
Mjerumani huyo, alitimiza mabao 67
akiwa Bayern Munich msimu wa 1972-1973.
Mabao ya Lio yanatokana na mabao
38 aliyofunga katika La Liga; mawili kwenye Kombe la Mfalme; matatu kwenye Supercopa,
moja kwenye Super Cup ya UEFA; mawili Klabu Bingwa ya Dunia na mengine 14 katika
Ligi ya Mabingwa.
0 comments:
Post a Comment