// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MCHEZAJI AZAM AFIA GESTI SINZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MCHEZAJI AZAM AFIA GESTI SINZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 23, 2012

    MCHEZAJI AZAM AFIA GESTI SINZA

    Baadhi ya wachezaji wa Azam

    RAIA wa Nigeria, Ferdinand Uzoma Onyenso(31), amekutwa amekufa katika chumba alichokuwa amepanga katika nyumba ya kulala wageni Fanaleki iliyopo Sinza wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mtu huyo alikutwa amekufa juzi saa 6:30 mchana katika chumba namba 110 huku maiti yake ikiwa imelala kitandani na haikuwa na jeraha lolote.
    Kenyela alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Onyenso alikuja hapa nchini kwa ajili ya
    shughuli za kimichezo kuchezea mpira wa miguu katika timu ya Azam FC iliyopo Ligi Kuu Tanzania Bara.
    Alisema chumba chake kilipopekuliwa ilipatikana hati yake ya kusafiria namba A03512586 iliyotolewa nchini Nigeria pamoja na hati ya Uhamiaji iliyotolewa hapa nchini yenye namba 01767922.
    Aidha alisema kuwa Onyenso alikuwa amepanga chumba hicho Aprili 20 na maiti yake imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa upelelezi zaidi.
    Wakati huohuo, Mwandishi Timzoo Kalugira anaripoti kuwa klabu ya Azam imedai Onyenso si mchezaji wake na wala haimtambui.
    Katibu Mkuu wa Azam, Nassoro Idrissa akizungumza na gazeti hili jana alisema kuwa wameshtushwa na taarifa hizo za polisi na kuomba ufanyike uchunguzi haraka ili kuweza kubaini ukweli halisi.
    “Hatuna mchezaji kutoka Nigeria ambaye tunataka kumsajili, inawezekana kuna watu wanatumia jina la timu yetu au walimchukua huyo mchezaji kwamba asubiri baada ya ligi wamtafutie timu, pengine ndiyo wamemwambia watamleta Azam.
    “Ni tukio la kusikitisha kibinadamu kwamba ametangulia mbele ya haki, lakini naomba uchunguzi ufanyike namna alivyoingia ili kubaini ukweli ni upi, lakini sisi Azam huwa mambo yetu tunapenda kuweka hadharani, huyo si mchezaji wetu,” alisema.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI AZAM AFIA GESTI SINZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top