Maugo juu ya mzani huku Cheka akiangalia |
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka
na Mada Maugo leo wamewapima uzito na
bondia Mada Maugo na Na
Francis Cheka wote wamekutwa na kilogramu 76.5 ambapo mpambano wao utafanyika
Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la
raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni
ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa
kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo
Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani
kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi
ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia
za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.
“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa
ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la
kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo
yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea
vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa
siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa
na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo
katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo
hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa
Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma
kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa
kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa
DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd
Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo
zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo
na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa
kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na
Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa
ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D.
CHEKA AKIWA NA WAPAMBE WAKE
MADA MAUGO NA CHEKA WAKINYOOSHWA MIKONO JUU NA PROMOTA
PROMOTA AKIWA NA MABONDIA HAO
Bondia Mada Maugo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa IBF na Francis Cheka kushoto mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kesho na mshindi atanyakua zawadi ya gari.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment