SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewateua waamuzi wanne wa
Tanzania kuchezesha mechi ya marudiano ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho kati
ya Black Leopards ya Afrika Kusini na Warri Wolves ya Nigeria itakayochezwa
nchini Afrika Kusini kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo amesema kwamba waamuzi hao ni Waziri Sheha atakayepuliza filimbi
wakati wasaidizi wake watakuwa John Kanyenye na Erasmo Jesse. Mwamuzi wa akiba
(fourth official) atakuwa Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Aurelio
Mathias wa Msumbiji.
Boniphace Wambura ameiambia bongostaz.blogspot.com leo kwamba
mechi ya kwanza kati ya timu hizo itachezwa Jumapili (Aprili
29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Warri City ulioko Jimbo la Delta nchini Nigeria
na itachezeshwa na waamuzi kutoka Senegal wakati Kamishna atakuwa Inyangi
Bokinda wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
0 comments:
Post a Comment