SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kwa mara nyingine limetoa adhabu kufuatia kufanyika kwa vitendo vya kihuni katika viwanja vya soka. TFF imezipiga faini za Sh 500,000 kila moja, timu za Mtibwa na Polisi Dodoma baada ya wachezaji na mashabiki wao kuhusika na vurugu za uwanjani. Kamati ya Ligi ya TFF imekwenda mbali zaidi na kumfungia mwamuzi Ramadhan Msangi wa Dodoma, ambaye aliboronga mechi ya Mtibwa na Azam. Pia imewafungia waamuzi wasaidizi wa mchezo huo, Samuel Mpenzu na Abdalla Uhako kutokana na kushindwa kumudu mchezo huo. Mambo haya yametokea katika kipindi ambacho mashabiki wa soka bado wana kumbukumbu za vurugu zilizotokea kwenye mechi baina ya Yanga na Azam. Mwamuzi wa mchezo huo, Israel Nkongo alipigwa na wachezaji wa Yanga, ambao hawakuridhika na uamuzi wake na timu hiyo ikafungwa 3-1. Kamati za TFF ziligongana juu ya hatua za kuchukua dhidi ya wachezaji wa Yanga ingawa hatimaye baadhi ya wachezaji waliadhibiwa. Kuna mambo mengi yanajitokeza kwa sasa, ambayo kimsingi yanafanya watu wajiulize kinachoendelea kwenye ligi. Mathalani, mechi tatu ambazo zinahusisha timu ya Azam zimemalizika kwa vurugu huku timu pinzani zikilalamikia kuonewa na waamuzi. Mechi hizi ni dhidi ya Yanga, Polisi Dodoma na mechi ya Mtibwa ndiyo haikumalizika kabisa kutokana na vurugu za uwanjani. Pia utata mwingine ni kuhusiana na uwezo wa waamuzi wenyewe katika uchezeshaji na uadilifu wao. Siyo siri, ligi ya mwaka huu ilianza vizuri na ilikuwa na ushindani mkali, lakini wakati huu ikielekea ukingoni imechafuliwa na kashfa za uchezeshaji mbovu zinazoendelea sasa. Hii inatokana na ukweli kuwa mechi nyingi za Azam zimeingiwa na doa la vurugu kiasi cha kuzua hoja kwamba timu hiyo inapendelewa ama kuna mchezo mchafu unaoendelea ili kuibeba. Sisi hatutaki kuingia kwa undani katika suala hilo, lakini bila shaka kuna haja ya kufanya uchunguzi na kujua kinachojiri kwenye ligi. Azam iliyoanzishwa mwaka 2004 siyo siri ina ukwasi mkubwa, na imetoa changamoto kubwa na hasa kwa Simba na Yanga ikiwa ndani na nje ya uwanja. Imesuka timu nzuri ya wakubwa na yosso na pia imefanya uwekezaji mkubwa kwa kujenga uwanja na hosteli. Hata hivyo, katika siku za karibuni kumekuwa na maneno mengi kuwa Azam wanabebwa na kwamba kuna harufu ya rushwa, sasa ili kuondoa dhana hii, tunashauri Kamati ya Ligi ya TFF kuchunguza tabia na vitendo vya waamuzi na hata klabu yenyewe. Kuna mawili, kama haijihusishi na vitendo vya rushwa, basi uchunguzi utaisafisha Azam na kuwapa watu moyo wa kuwekeza katika soka na pia kama kuna ukweli kuwa waamuzi wananunuliwa, basi kutasaidia kusafisha soka letu. Kinachosikitisha ni kuwa, suala la rushwa katika soka yetu limekuwa likifumbiwa macho kwa muda mrefu na sasa linatutafuna. Hali hii imefanya wadau wa soka kutoamini matokeo ya uwanjani katika mechi za Ligi Kuu Bara kwa kuwa suala la rushwa limegeuzwa kuwa sehemu ya utaratibu wa kuendesha soka letu. Ndiyo maana siyo ajabu siku hizi timu zetu zinatolewa mapema kwenye mashindano ya klabu barani Afrika kwa kuwa bingwa anapatikana kwa kununua mechi, na hili siyo siri. Kamati ya Ligi pia inapaswa kuangalia jinsi ya kukuza kiwango cha elimu ya waamuzi, kwani uchezeshaji wa ligi yetu bado uko chini. Nchi yetu haina waamuzi wa daraja la akina Gratian Matovu, Abdalla Rajab, Hafidh Ally, Mfaume Ally, Zuberi Bundala, Juma Ally David, Taji Bakari na Mussa Lyaunga waliokuwa waamuzi wa kiwango cha juu. GAZETI LA MWANASPOTI: |
OG Anunoby Impresses NBA Fans vs. Former Team as KAT, Knicks Beat Barrett,
Raptors
-
Karl-Anthony Towns and OG Anunoby each scored 27 points to lead the New
York Knicks to a 112-98 home win over the Toronto Raptors on Wednesday.
Towns retur...
25 minutes ago
0 comments:
Post a Comment