Balotelli |
KOCHA
wa Manchester City, Roberto Mancini anazinguliwa mno na mshambuliaji mtata,
Mario Balotelli kiasi kwamba anasema kama angekuwa anacheza naye, angeishia
kumpiga.
Mtaliano
huyo alizungumza kabla ya skendo jipya la Balotelli kupata ajali Alhamisi akiwaambia
Waandishi wa Habari kwamba hazungumzi na Mtaliano mwenzake huyo kila siku, kwa
sababu kama angefanya hivyo ingebidi amuone mtaalamu wa phycholog.
Mancini,
anayeiandaa timu yake kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu, ambao wanatakiwa lazima
washinde dhidi ya Arsenal Jumapili, amesema sasa ameona kwa nini wachezaji
wenzake Balotelli wanazinguliwa naye.
"Naweza
kuelewa hii. Nilimuambia kama ungecheza na mimi, miaka 10 iliyopita, ningekuwa
nakupiga kichwani kila siku," alisema Mancini.
"Nawaelewa
wachezaji wenzake, lakini kuna njia tofauti za kuwasaidia vijana kama Mario. Katika
kila mechi kubwa, amekuwa akicheza vizuri sana. Tatizo lake ni fikrab zake
mchezoni, lakini nafanya naye kazi kila siku (juu ya hilo).
"Nazungumza
naye – siyo kila siku, kwa sababu ningehitaji mtaalamu wa psychology – lakini kila
siku mbili nazungumza naye. Hapotezi ubora wake. Mario, kama mchezaji, anaweza
kuwa mmoja (wachezaji) babu kubwa Ulaya.
Sitaki apoteze kipaji chake."
Balotelli,
mwenye umri wa miaka 21, ambaye amekuwa akitawala vichwa vya habari kwa muda
mrefu, aliibuka tena jana kwenye kurasa za mbele juu ya maisha yake binafsi
baada ya kupata ajali akiwa anaendesha gari lake.
Mshambuliaji
huyo ambaye anaendesha Bentley, alitoka salama kwenye ajali hiyo na anatarajiwa
kucheza Jumapili, lakini Polisi imethibitisha abiria mmoja katika gari mbili
zilizohusika kwenye ajali alipelekwa hospitali.
Taarifa
kutoka Polisi ya Jiji la Manchester ilisema: "Muda mfupi baada ya saa 9.15
jioni Alhamisi, Aprili 5, 2012, polisi walipigiwa simu kuitwa Mtaa wa Medlock, katikati ya Jiji la Manchester
kuchukua taarifa ya ajali iliyohusisha gari mbili.
"Abiria
mmoja kutoka kwenye gari hizo mbili alipelekwa hospitali kwa matibabu. Uchunguzi
unaendelea."
Balotelli,
ambaye mapema msimu huu alisababisha ajali ya moto nyumbani kwake baada ya
kufungia ndani vifaa vya kudhibiti moto akiwa amevizima, amekuwa akitawala
magazeti wiki mbili hizi baada ya kuibuka ghafla kwenye mkutano na Waandishi wa
Habari wa klabu yake ya zamani, Inter Milan kumtambulisha kocha wake mpya.
Pia
aligombana na kocha wake Mancini mazoezini mwishoni mwa wiki iliyopita, na
akagombea na mchezaji mwenzake Aleksandar Kolarov kupiga mpira wa adhabu katika
sare ya 3-3 waliyolazimishwa na Sunderland.
Licha
ya kufunga mabao mawili siku hiyo, uchezaji wa Balotelli ulipondwa na Mancini, ambaye
alisema alitaka kumtoa baada ya dakika tano tu.
Pamoja
na hayo, Mancini bado ana matumaini na mchezaji huyo ambaye amekuwa akimuona
tangu angali kinda kabisa Italia.
Mancini
alisema: "Kuna watu ambao wanafikiri vibaya tu juu ya watu wengine, kama
Mario. Kila wakati Mario kafanya kitu fulani, ni kama vita.
"Kuna
watu wengine ambao ndani na nje ya Uwanja wanafanya madhambi zaidi ya Mario na
hakuna hata mmoja anayesema chochote, labda kwa sababu wanachezea timu muhimu
au hawako kama Mario."
0 comments:
Post a Comment