Bobana wa Simba katika moja ya mechi za Ligi Kuu |
LIGI Kuu ya Vodacom Tanazania Bara inaendelea katika raundi
ya 25 kesho (Aprili 28 mwaka huu) ambapo Coastal Union itakuwa mwenyeji wa
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa
mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.
Aprili 30 mwaka huu Azam na Toto African zitacheza Chamazi
wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa
Chamazi.
Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu
ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro
JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Ruvu Shooting vs
Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).
Mechi nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union vs Toto
African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam
vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar
(Jamhuri, Morogoro).
0 comments:
Post a Comment