Kikosi cha Yanga |
Dar es Salaam, kuanzia Juni 23 hadi Julai 7 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amethibitisha kwamba michuano hiyo kwa mara nyingine tena itafanyika jijini Dar es Salaam, baada ya kufanyika kwa mafanikio zaidi mwaka jana.
Kwa mujibu wa Musonye, kufanyika kwa michuano hiyo nchini Tanzania ni kutokana kuwa na
uhakika wa udhamini mkubwa.
Bingwa mara 12 wa Ligi Kuu ya Rwanda na bingwa mara nne wa Kombe la Kagame, APR, ambayo imekiimarisha kikosi chake msimu huu, licha ya kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imejipanga kulitwaa kombe hilo kwa mara ya tano.
Mwaka jana APR na Etincelles zilitolewa hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Mwaka jana Yanga ilitwaa taji la michuano hiyo kwa kuifunga Simba kwa bao 1-0 hatua ya fainali, ambapo Yanga ilikuwa ikinolewa na Mganda Sam Timbe ambaye hilo lilikiwa ni taji lake la nne la Cecafa, baada ya kulibeba mwaka 2009 akiwa na Atraco, Polisi Uganda (2006)
na SC Villa (2005).
Rais Paul Kagame amekuwa akidhamini kombe hilo kwa zawadi za washindi kwa dola 60,000 sawa na shilingi 93,600,000.
0 comments:
Post a Comment