// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOCHA WA YANGA AWAPA SIMBA SIRI ZA AL AHLY SHANDY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOCHA WA YANGA AWAPA SIMBA SIRI ZA AL AHLY SHANDY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 24, 2012

    KOCHA WA YANGA AWAPA SIMBA SIRI ZA AL AHLY SHANDY



    SREDOJEVIC MILUTIN MICHO
    AL-AHLY Shandy ya Sudan itakayokutana na Simba kwenye raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho inashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano ya klabu barani Afrika.

    Makao makuu ya timu hiyo yapo katika Mji wa Shandy, ambao upo kilometa 100 kutoka mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
    Si timu ya kubeza licha ya kutokuwa na ukubwa wa timu vigogo za Sudan za Al-Hilal na Al-Merreikh.

    Hii inatokana na ukweli kuwa, imedhihirisha makali yake baada ya kuitoa Ferroviaro ya Msumbiji kwenye raundi ya kwanza ya mashindano haya.

    Ferroviaro ina uzoefu mkubwa katika mashindano haya kwani imewahi kufuzu kwa hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Simba itakabiliana Al-Ahly Shandy, Aprili 29 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza.

    Shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari limeteua waamuzi kutoka Swaziland, Nhleko Simanga Pritchard atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Mbingo Petros Mzikayifani na Sibandze Thulani. Mwamuzi wa mezani atakuwa Fakudze Mbongiseni Elliot.

    CAF pia imemteua Kayijuga Gaspard wa Rwanda kuwa Kamishina wa mechi hiyo.

    Al Ahly imepata nguvu kutokana na jeuri ya fedha ya tajiri wa Sudan, Salah Idris, ambaye aliwahi kuongoza timu kigogo ya Al-Hilal kwa miaka nane.

    Salah anatokea katika Mji wa Shandi na aliisaidia timu hiyo kupanda daraja mwaka jana, na iliposhiriki tu kwa mara ya kwanza ikakata tiketi ya kushiriki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.

    Alipokuwa Al-Hilal aliisaidia kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka ya 2007 na 2009.

    Tajiri huyo aliamua kuachana na Al-Hilal na kugombea uongozi wa Shirikisho la Soka la Sudan, ingawa alishindwa kwenye uchaguzi wake.

    Salah amemwajiri kocha kutoka Tunisia, Kuki na nyota wa kigeni kutoka nchi za Nigeria, Mali na Saudi Arabia katika kikosi cha Al-Ahly Shandy.

    Al Ahly ina raia wawili wa Nigeria, beki wa kati, Malik Isaac na Ike Francis, ambaye ni mfungaji hatari.
    Kuna kiungo kutoka Mali, Bashiru na kipa Abdulraham Ali Daya, ambaye kwao ni Saudi Arabia.

    Tajiri huyo wa Al Ahly pia aliwasajili wachezaji waliotemwa na Al-Hilal, ambao ni mabeki Osama Tawoon, Sadam Abdutalib, Samu Abdalla na wachezaji wa kiungo, Hamooda Bashir na mshambuliaji Nadir Al Taib, ambaye ndio alifunga mabao mawili wakati timu hiyo ilipoitoa Ferroviaro ya Msumbiji kwenye raundi ya kwanza.

    Wachezaji hawa wa kigeni ukijumlisha na wachezaji wa zamani wa Al-Hilal, ambao wana uzoefu mkubwa na mashindano ya Afrika kunaifanya timu hiyo kuwa tishio kwa Simba.

    Al-Ahly, ambayo inashika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu Sudan inajivunia vitu vikubwa vitatu.

    Jamaa wanajiamini na hawaiogopi Simba kwani wanajivunia fedha nyingi na wanawalipa wachezaji wao vizuri, pia wana wachezaji wenye vipaji na kikosi chao kimesheheni wazoefu.
    Pia wamepania kumdhibiti mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu kwani wanafahamu kutokana na kuwahi kuchezea Al-Hilal ya Sudan.

    Kutokana na mazingira haya kunafanya Al-Ahly kuingia huku ikijiamini kwenye mechi hizi dhidi ya Simba.
    Simba sasa watapaswa kujipanga kwa mbinu zote ndani na nje ya ili kuing'oa Al-Ahly kama ilivyofanya kwa Entente Setif ya Algeria.

    Mwandishi wa makala hii ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda, na amewahi kuifundisha Yanga.

    GAZETI LA MWANASPOTI LEO:
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA WA YANGA AWAPA SIMBA SIRI ZA AL AHLY SHANDY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top