Pasquale Marino |
GENOA imemfukuza kocha wake Pasquale Marino na kumteua Alberto
Malesani, ambaye anakuwa kocha wa 17 kufukuzwa katika Ligi Kuu Italia, Serie A yenye
kushirikisha timu 20, tangu kuanza kwa msimu huu.
Genoa ilitangaza hatua hiyo Jumatatu, timu hiyo ikiwa
inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa imecheza mechi tisa
bila kushinda, ya mwisho wakifungwa 5-4 na Inter Milan Jumapili. Hiyo inahusisha
kufungwa mechi tano na sare nne.Malesani alifukuzwa Desemba baada ya kipigo cha 6-1 kutoka kwa Napoli, lakini Genoa ilikuwa inalingana kwa pointi na timu inayoshika nafasi ya tisa kwenye ligi wakati huo.
0 comments:
Post a Comment