Simba kazi moja leo Imeandikwa na Clecence Kunambi; Tarehe: 28th April 2012 @ 14:59 Imesomwa na watu: 141; Jumla ya maoni: 0 |
Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa waliingia kwenye hatua hiyo baada ya kuiondoa kwenye mashindano hayo timu ya Entente Setif ya Algeria ugenini kwa faida ya bao la ugenini baada ya timu hiyo ya Algeria kushinda nyumbani kwa mabao 3-1. Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Kabla ya kukutana na Setif, Simba iliiondoa kwenye mashindano hayo timu ya Kiyovu ya Rwanda kwa mabao 3-2, hiyo ni kutokana na kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa Kigali, Rwanda na zilipokuja kurudiana Dar es Salaam Simba ilishinda kwa mabao 2-1. Al Ahly SDhandy mpaka kufikia hatua hiyo iliitoa timu ya Ferroviario ya Msumbiji na sasa inakabiliana na vinara hao wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara ugenini. Mshindi baina ya timu hizo kwenye mechi ya leo atajiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua inayofuata kwani timu hizo zitarudiana baada ya wiki mbili Khartoum Sudan. Ni mechi inayokutanisha timu mbili zenye mazingira tofauti kwenye mashindano hayo kwani Simba ina uzoefu na historia nzuri na mashindano hayo kwani mbali na kushiriki mara kadhaa, lakini pia iliwahi kufika hatua ya fainali na kulikosa kombe nyumbani kwa kufungwa mbao 2-0 na Stella Abdijan ya Ivory Coast mwaka 1993. Al Ahly Shandy ni timu ndogo isiyo na historia yoyote kwenye mashindano hayo kwani hii ni mara ya kwanza kushiriki. Mara nyingi Sudan imekuwa ikiwakilishwa na timu za El Hilal na El Merreikh kwenye mashindano makubwa ya Afrika. Kutokana na mazingira hayo, mchezo wa leo unagusa hisia tofauti tofauti miongoni mwa wadadisi wa mambo ya soka la Tanzania, kwani wapo watakaokuwa wanaamini Simba itakuwa na kazi rahisi dhidi ya Wanubi hao, lakini wapo pia watakaokuwa wanaamini mchezo wa leo hautabiriki na lolote linaweza kutokea. Lakini uhalisia wa mchezo wa soka ni kwamba hata siku moja haitabiriki pamoja na juhudi za wachambuzi wa mchezo huo kujaribu kutabiri matokeo yake mara kwa mara. Hivyo mechi hiyo ni ngumu na mwamuzi bado ataendelea kuwa dakika 90 za mchezo huo. Simba wanatakiwa kuupa uzito mkubwa mchezo wa leo ikibidi kupata mabao mengi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri pindi timu hizo zitakaporudiana wiki mbili zijazo nchini Sudan. |
Peter Crouch and Joleon Lescott give their verdict on Pep Guardiola's
future and Man City's title chances after a sixth defeat in eight Premier
League games
-
Peter Crouch and Joleon Lescott have provided their verdict on Pep
Guardiola's Manchester City future following his side's latest setback.
City were beaten...
19 minutes ago
0 comments:
Post a Comment