// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIFO CHA BARCA NI LEO CAMP NOU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIFO CHA BARCA NI LEO CAMP NOU? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 03, 2012

    KIFO CHA BARCA NI LEO CAMP NOU?

    San Siro ilikuwa hivi, Camp Nou itakuwaje?

    KUELEKEA mchezo wa leo wa robo fainali ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Barcelona iliwapumzisha wachezaji wake kibao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao Jumamosi usiku, lakini Carles Puyol anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya AC Milan, Nahodha huyo wa Catalan akicheza pacha na Gerard Pique katika safu la ulinzi.

    Xavi pia alikuwa nje kwenye mechi ya mwishoni mwa wiki na anasumbuliwa na misuli, ambayo inamaanisha hajawa fiti kiasi cha kutosha, Thiago anaweza kukamata nafasi ya kiungo.
    Beki Eric Abidal na mshambuliaji David Villa, wakati huo huo, wanaendelea kuwa nje ya kikosi.
    Beki wa kushoto Adriano pia alirejea kazini baada ya kupona majeruhi na alicheza dhidi ya Athletic na anatarajiwa kucheza kwenye kikosi cha leo na kocha Pep Guardiolaamethibitisha kiungo Cesc Fabregas atakuwepo tena baada ya kupona mgongo. Nyota huyo wa zamani wa Arsenal anagombea nafasi dhidi ya Pedro ili kucheza na Lionel Messi, ambaye aliwekewa ngumu na safu ya ulinzi ya Rossoneri kwenye mechi ya kwanza, na Alexis Sanchez.
    Kocha wa Milan, Massimiliano Allegri alitaraji kuwa na kiungo Mark van Bommel baada ya kuikosa mechi ya kwanza kwa sababu ya adhabu, lakini mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 hakujumishwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 kutokana na kuwa majeruhi, hivyo Massimo Ambrosini atacheza tena.
    Thiago Silva ataendelea kuwa nje kwa sababu hajapona misuli, hivyo mkongwe Alessandro Nesta atasimama tena kwenye beki ya kati kufuatia kucheza vizuri mechi ya kwanza San Siro wiki iliyopita.
    Nguvu mpya katika kikosi cha Rossoneri ni kwamba, Alexandre Pato, ambaye alifunga katika sare ya 2-2 Uwanja wa Camp Nou kwenye ya hatua ya makundi baina ya timu hizo, amepona misuli baada ya kutibiwa Marekani na yumo kwenye kikosi cha leo.
    Mbrazil huyo ameelezewa yuko tayari kucheza, ingawa anaweza kutokea benchi huku Zlatan Ibrahimovic na Robinho wakitazamiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji.
     

    JE WAJUA?
    •Barcelona haijafungwa nyumbani kwenye michuano ya Ulaya tangu Oktoba mwaka 2009, ilipofungwa 2-1 na Rubin Kazan.
    •Mechi ya kwanza ilikuwa sare ya 0-0 na Milan imekuwa timu ya kwanza katika mechi 30 kukilazimishwa sare ya bila mabao kikosi cha Guardiola Ulaya.
     •Kama Messi atafunga, atafunga rekodi ya mabao 12 kwa msimu kwenye Ligi ya Mabingwa, ambayo kwa sasa anaishikilia kwa pamoja na Ruud van Nistelrooy.
     •Rekodi ya AC Milan kwa Barca ni kushinda mechi nne, sare tano na kufungwa tano kwenye michuano ya Ulaya.
     •Kikosi cha Allegri haijashinda mechi ya ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, kimetoa sare tatu na kufungwa mechi moja.
     •The Rossoneri waliikung’uta Barcelona mabao 4-0 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Athens, Ugriki mwaka 1994.

    VIKOSI VYA LEO:
    BARCELONA: Valdes, Dani Alves, Pique, Puyol, Adriano, Thiago, Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi na Cesc.
    AC MILAN: Abbiati, Abate, Nesta, Mexes, Antonini, Seedorf, Ambrosini, Nocerino, Boateng, Ibrahimovic na Robinho.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIFO CHA BARCA NI LEO CAMP NOU? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top