// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIFAA CHA KWA KABILA CHATUA MSIMBAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIFAA CHA KWA KABILA CHATUA MSIMBAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 01, 2012

    KIFAA CHA KWA KABILA CHATUA MSIMBAZI


    DORIS MALIYAGA na OLIVER ALBERT
    KIUNGO wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Patrick Kanu Mbiyavanga ameanza mazoezi rasmi na Simba juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa TCC

    Chang'ombe jijini Dar es Salaam na ameahidi kufanya kazi nzuri kuhakikisha kikosi hicho kinafikia malengo.

    Mwanaspoti lilikuwa gazeti la kwanza nchini, kuripoti habari za usajili wa Mbiyavanga na Mussa Mude wa Sofapaka katika klabu ya Simba. Habari hizo ziliripotiwa na Mwanaspoti tangu mwanzoni mwa Februari.

    Mbiyavanga aliivutia Simba baada ya kumwona akiwa na kikosi cha DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwenye Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

    Kiungo huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na alishawahi kuichezea klabu ya GD Inter Luanda inayoshiriki Ligi Kuu Angola, aliiambia Mwanaspoti kuwa amejiunga Simba kwa sababu anaipenda na tayari amesaini mkataba wa miaka miwili.

    "Tulikubaliana na viongozi na malengo yangu ni kufanya kila niwezalo kuona naisaidia Simba kufikia malengo yao," alieleza Mbiyavanga.
    Kocha wa Simba, Milovan Corkovic alisema hajamwona Mbiyanga akicheza mechi lakini anaamini ni mchezaji mzuri.

    Kimsingi Mbiyavanga alivutwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa Simba, Moses Basena.
    Basena alivutiwa na mchezaji huyo baada ya mechi kati ya Simba na Motema Pembe, mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Basena aliweka wazi alikuwa amevutiwa naye mbele ya waandishi wa Mwanaspoti na ndilo lilikuwa gazeti la kwanza kuripoti kuwa mchezaji huyo atajiunga na Simba.
    Katika hatua nyingine, kiungo huyo juzi Alhamisi alionja joto ya jiwe mbele ya kocha Milovan Cirkovic baada ya kuleta maringo mazoezini.

    Aliingia uwanjani hapo na kuwakuta wachezaji wote wa Simba wameshaanza mazoezi, lakini alitakiwa kuanza kukimbia kuzunguka uwanja.

    Alitii amri hiyo lakini alikuwa anakimbia huku akiwa ameshusha kaptula yake kwa mtindo wa 'mlegezo�.
    Baada ya kukimbia raundi mbili, uvumilivu ulimshinda Cirkovic na mchezaji huyo alipofika karibu yake alimuita na kumtaka kupandisha kaptula yake huku akimkaripia kuwa hataki tabia za kihuni.

    �Pandisha kaptula hiyo,� alisikika Cirkovic na mchezaji huyo alipandisha kidogo na kuendelea kukimbia, lakini kocha huyo akamwamuru arudi na kumtaka kupandisha vizuri hadi juu ndipo aendelee kukimbia, kitu alichokitekeleza na kisha kuendelea na mazoezi na kuwaacha watu wakiangua kicheko.


    GAZETI LA MWANASPOTI:
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIFAA CHA KWA KABILA CHATUA MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top