Kaseba kulia akisaini kuzipiga na Cheka. Kushoto ni promota Kaike Siraju |
BINGWA wa zamani wa Kick Boxing, Japhet Kaseba amesaini
mkataba wa kucheza na Bingwa wa dunia wa ndondi wa IBC, Francis Cheka wa
Morogoro katika pambano la uzito wa Middle, Julai 7, mwaka huu Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Kaseba amesema
anashukuru kupata mpambano huo na atahakikisha anaonyesha uwezo wake wote
katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano
“Najua mabondia wa hapa bongo wananikwepa sana kwa kuwa
nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke, lakini hawajui mimi ni bingwa katika
mapigano yote,” alisema Kaseba.
“Nitahakikisha naweka kambi ya kutosha na kukata ngebe za Cheka,
ni mtoto mdogo sana katika masumbwi kwa kweli bingwa wa kweli ni Rashid Matumla
ambaye ninamuheshimu, mpaka sasa Cheka kanikimbia muda mrefu tu tangu tupambane
mara ya kwanza (Oktoba 3, 2009),”alisema Kaseba.
Cheka alishinda pambano la kwanza kwa Technical Knockout (TKO),
lakini Kaseba anadai alipewa ubingwa kwa kusingizia mashabiki wake walimtupa
nje ya ulingo.
“Kazi yake yeye anarudiana na Mada Maugo kila siku, lakini
kwa sasa kakanyaga miwaya zamu yake imefika,”alisema.
Naye Promota wa mpambano huo, Kaike Siraju
amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam katika ukumbi ambao mutatajwa
baadaye.
0 comments:
Post a Comment