Published: Today at 09:34
KIM Kardashian na Kanye West walitoka kwa chakula cha usiku wakiwa wameshikana mikono kimahaba – bila ya kuhjofiua wala kujali lolote.
Wawili hao wamekuwa wakijificha mno katika mapenzi yao, lakini wameamua kujiachia baada ya katika hafla ya uzinduzi wa mgahawa wa Scott Disick, New York Restaurant.
Walionekana waliopendeza ile mbaya, kimwana akiwa amevalia ganu jeusi na viatu vya mchuchumio vyeusi.
Alionekana mtulivu, lakini mwenye furaha wakati kamera ikiwanasa wapendanao hao walipokuwa wakiingia pamoja wameshikana mikono.
Kim, mwenye umri wa miaka 32, alianza kula uroda na rapa huyo mwenye umri wa miaka 34 mwanzoni mwa mwezi, lakini rasmi hawajathibitisha kwamba ni wapenzi.
Kanye hivi karibuni ametoa wimbo mpya kuhusu kuzama kwenye penzi la mlimbwende fulani, wakati anaonekana akiwa pamoja na aliyekuwa mke wa Kris Humphries.
Aliimba: “Na ninasema nimezama kwenye penzi la Kim, katika wakati huo huo amezama kwenye penzi lake.
“Safi, hiyo poa mtoto wa kike, fanya mambo yako.”
Kim amefungua kesi ya kuomba talaka kwa mchezaji huyo wa mpira wa kikapu Oktoba, baada ya siku 72 za ndoa yao.
Usiku wa jana, Kanye aliamua kumpa kampani mwanamke wake mpya katika shughuli ya shemeji yake na alikuwa amepiga suti moja kali na viatu vya nguvu.
Lakini ndani alikuwa amepiga fulana ya ranfu kama ya kijivu.
Tukio hilo lilikuwa la kifamilia wakati dada yake Kim, mjamzito, Kourtney – alionekana katika gauni jeusi lenye weupe – akiwa na mumewe.
Khloe naye alikuwa bomba na mumewe Lamar Odom aliyekuwa amevaa suti ya kijivu na shati la bluu.
wakati huo huo, Kim alipata muda wa kujiachia na wasichana wenzake.
Aliweka picha kwenye tweeter akiwa na rafiki wa Khloe, Malika, usiku huo Los Angeles, kabla ya kupaa kwenda New York kuungana na Kanye.
0 comments:
Post a Comment