Kalou |
Wachambuzi wengi wanaipa Barca
nafasi kubwa ya kuifunga The Blues na kuingia fainali kwa mara ya tatu ndani ya
miaka minne, lakini Kalou anasema safu ya ulinzi ya Pep Guardiola ina makosa ya
kutosha kuwapa matumaini ya kuwatoa mabingwa hao watetezi.
Wakati ubora wa Barca umelalia
kwa wanasoka bora duniani, Lionel Messi, Andres Iniesta na Xavi, nyota huyo wa Ivory
Coast, Kalou havutiwi sana na beki nne yao.
"Wana udhaifu," Kalou alisema.
"Tunafahamu hawakuwa wenye kujiamini sana katika safu ya ulinzi,
wamefungwa mabao mengi, hivyo hilo ndilo jambo ambalo tutalitumia.
"Watu wanaona jinsi Barcelona
inavyocheza leo na wanaweza kusema, 'Chelsea haina nafasi dhidi ya Barcelona'.
"Lakini, kama mchezaji wa Chelsea,
tunajituma kila siku mazoezini na tunaamini kwamba uwanjani ndio sehemu pekee
ya majibu juu ya dhana zote hasi. Mashabiki wetu wanatarajia tutashinda, tunatarajia
ushindi."
Pamoja na kwamba Barcelona inapewa
heshima kubwa sana Ulaya hivi sasa, Kalou anasema kushindwa kwao kumbana Jose
Mourinho na timu yake Real Madrid katika
Ligi ya Hispania msimu huu, inathibitisha kwamba si wagumu.
"Kila mmoja anasahau kwamba
Madrid wana msimu babu kubwa na Jose," alisema Kalou.
"Hata sasa, kama tungecheza
na Madrid, watu wasingesema kwamba Chelsea haina nafasi.
"Lakini, kwa sababu ni Barca,
kwa sababu wanaye Messi na wachezaji wote hao, watu wanafikiri kwamba hatutuwawezi.
"Wachezaji wa Chelsea wanafahamu
kwamba huu ni mchezo mmoja, kwenye mchezo mmoja, kitu chochote kinaweza kutokea."
Kalou na wachezaji wenzake pia
wameonyeaha nia ya kushinda ili kupoza machungu yao walipokutana na Barca mara
ya mwisho na kufungwa kwa utata kwenye Nusu Fainali mwaka 2009.
The Blues ilistahili kupewa penalti
kadhaa za wazi zilizokataliwa na refa kabla ya Iniesta kufunga bao la ushindi
dakika ya mwisho.
Kalou, ambaye alikuwa benchi tu
muda wote wa mchezo huo, anaikumbuka mechi hiyo vizuri sana.
0 comments:
Post a Comment