Torres katika mechi ya kwanza na Benfica |
MSHAMBULIAJI wa Ivory
Coast, Didier Drogba anaweza kuwa nje baada ya kukosa mechi dhidi ya Aston
Villa Jumamosi kutokana na kuwa majeruhi, wakati Raul Meireles anayeumwa goti, naye
pia hakucheza Villa Park, anakabiliana na ushindani wa namba dhidi ya Frank
Lampard, Ramires na Michael Essien kuanza katika nafasi ya kiungo.
David Luiz aliuamia kifundo cha mguu kwenye mchezo huo naye
huenda asichezee, Gary Cahill anatarajiwa kuchukua nafasi ya Mbrazil huyo baada
ya kumpisha kwenye mechi na Villa. Kule mbele, uamuzi pekee haswa wa kocha Roberto Di Matteo aidha kuwapanga Daniel Sturridge au Salomon Kalou, pamoja na hayo anaweza kuchagua kuongeza kiungo, itategemea na mipango yake katika mechi hiyo.
Wageni wanakabiliwa na janga la majeruhi kwa wachezaji wake kadhaa wa kikosi cha kwanza kutemwa kwenye safari ya London.
Mabeki Ezequiel Garay, Jardel na Miguel Vitor wote wapo wataikosa mechi hiyo kutokana na majeruhi, wakimuachia kiungo mkabaji Javi Garcia nafasi ya kuanza katika beki ya kati.
Wakati huo huo, nyota chipukizi Luis Martins, Andre Almeida na Ruben Pinto wamesafiri na kikosi cha kwanza.
JE WAJUA?
•Chelsea imeshinda kila mechi katika Ligi ya Masbingwa msimu huu.
•The Blues wamefunga mabao 14 Stamford Bridge, wakati wao wamefungwa moja tu, ambayo ni rekodi nzuri kuliko timu yoyote.
•Hakuna timu ya England daima iliyoshindwa kusonga mbele baada ya kushinda mechi ya kwanza ugenini.
•Ukiondoa mechi za kufu, wenyeji wamefunga bao katika mechi 10 mfululizo Ulaya kwa mara ya kwanza, walishinda mechi nne mfululizo zilizopita.
•Timu hiyo ya Ligi Kuu imetangulia kufunga katika kila mechi katika mechi zake tisa zilizopita za Ligi ya Mabingwa msimu huu.
•Benfica imeshindwa kupata ushindi mbele ya timu za England katika mechi tano zilizopita.
•Kiungo wa Argentina, Nicolas Gaitan ameingia kwenye orodha wa watoa pasi za mabao wakali kwenye michuano hiyo sambama na Karim Benzema wa Real Madird (5).
•Wageni wamefunga mabao nane kipindi cha kwanza katika mabao yao 12, ambayo ni idadi kubwa kuliko timu yoyote msimu huu kwenye michuano hii.
•Mechi ya kwanza ambayo Di Matteo aliiongoza The Blues kushinda 1-0 ugenini, ilikuwa ya kwanza Benfica inashindwa kutikiza nyavu katika Ligi ya Mabingwa msimu huu.
• David Luiz, Ashley Cole na Raul Meireles wa Chelsea walipata kadi za njano ugenini na wako hatarini kukosa Nusu Fainali. The Eagles pia hawana zaidi ya watano Artur, Ezequiel Garay, Luisao, Bruno Cesar na Javi Garcia wenye majina makubwa.
VIKOSI VYA LEO:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Lampard,
Essien, Ramires Mata, Torres na Sturridge.Benfica: Artur, Maxi Pereira, Luisao, Javi Garcia, Emerson, Matic, Bruno Cesar, Aimar, Gaitan, Cardozo na Rodrigo.
0 comments:
Post a Comment