Cisse akifunga |
KLABU ya Newcastle United
imezidi kujiongezea matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaysa msimu ujao,
baada ya kuichapa mabao 2-0 Swansea City, shukrani wake Papiss Cisse aliyefunga
mabao hayo yote.
Mshambuliaji huyo Senegal aliye
kwenye ‘fomu’ ya juu aliwafungia bao la kwanza The Magpies mapema tu baada ya
kuikimbilia pasi ya Yohan Cabaye na kumtungua kipa wa Swans, Michel Vorm akiwa
umbali wa yadi 20.
Swansea ‘Barca ya England’ ilitawala
mchezo, lakini Newcastle ilicheza kwa mipango zaidi na kufanikiwa kupata walichokuwa
wakihitaji. Ushindi huo wa nne mfululizo kwa
Newcastle unakihakikishia kikosi
cha Alan Pardew kuipiku Chelsea katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi
Kuu, ikizidiwa pointi mbili tu Tottenham Hotspur na Arsenal, ambao wanakalia
nafasi mbili za mwisho za kucheza Ligi ya Mabingwa.
Lakini Newcastle imejiwekea
matumaini ya kurejea kwenye michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa
2006-2007, kikosi cha Pardew kikiwa katika kiwango kizuri zikiwa zimebaki mechi
sita, wakati Cisse, ambaye sasa amefunga mabao tisa katika mechi nane tangu
asajiliwe Januari.
Swansea, wakati huo huo imefungwa
mechi tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tano wafungwe na York, Bury na Lincoln katika
Daraja la Kwanza Januari mwaka 2003.
DATA ZA MUHIMU SWANSEA v
NEWCASTLE
•Newcastle haijafungwa na Swansea
tangu Desemba 1980
•Swansea imeshindwa kushinda au
kufunga bao dhidi ya timu za Kaskazini Mashariki katika mechi nne msimu huu.
•Bao la tisa la Papiss Cisse
mwaka 2012 amekwenda sawa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney
•Hii ni mara ya pili kocha wa Newcastle,
Alan Pardew anashinda mechi nne mfululizo kama kocha wa Ligi Kuu, nyingine
alishinda alikuwa akiwa West Ham Januari na Februari 2006
•Ushindi huu wa Newcastle ni wa
kwanza kwa mechi za ugenini kwenye za Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment