China kushoto akiwa BIN ZUBEIRY kulia |
KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Abdallah
China amesema kwamba anasikitika jinsi ambavyo soka ya Tanzania inazidi
kuporomoka, wakati haoni jitihada za kuikwamua.
“Hali ya sasa inasikitisha, naambiwa sasa hata wachezaji wa
nafasi ya kiungo ni tabu, yaani watoto wa siku hizi sijui wanafanya nini.
Nadhani ni starehe sana, hawana mazoezi. Hawawezi kucheza
mpira namna hii, na hii ni kwa sababu hakuna misngi mizuri. Wachezaji hawajitambui
na hawana malengo, wanacheza tu basi,”alisema China.
China anayeishi London, Uingereza yupo nchini kwa muda kwa
ajili ya masuala ya kifamilia tangu juzi na anatarajiwa kuondoka Jumapili.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga na Simba SC, alisema kwamba
kazi kubwa lazima ifanyike ili soka ya Tanzania irudi kwenye heshima yake,
vinginevyo hali itazidi kuwa mbaya zaidi.
“Tuna bahati tuna rais anayependa michezo, lakini
tumeshindwa kumtumia. Nafasi hii
tutaijutia sana, akiondoka huyu (Jakaya Kikwete) kumpata rais mwingine mpenda
michezo kama yeye, itachukua muda sana,”alisema.
0 comments:
Post a Comment