Chicharito |
WAKATI michuano ya CONCACAF kuwania tiketi ya kucheza Olimpiki
imemalizika na Mexico imefuzu kushiriki michezo hiyo ya London mwaka huu, sasa
watu wanataka kusikia kikosi cha wachezaji 18 kitakachoiwakilisha nchi hiyo
kwenye michuano hiyo, hasa kujua hatima ya mchezaji mmoja tu.
Ni nyota wa Manchester United, Javier "Chicharito"
Hernandez ambaye ni mchezaji maarufu zaidi wa Mexico, na anatarajiwa kuichezea
nchi yake katika Olimpiki. Mshambuliaji huyo nyota, anakubalika mbele ya kocha Luis Fernando Tena.
"Chicharito anagombea nafasi. Kila mmoja anafahamu juu yake, kipaji chake, anacheza England," alisema Tena baada ya timu yake kuifunga Honduras 2-1 katika muda wa nyongeza na kutwa ubingwa wa CONCACAF U-23.
Hernandez atafikisha miaka 24 Juni, mwaka huu na kumfanya avuke umri wa kucheza Olimpiki.
Hivyo ataingia kwenye Olimpiki katika orodha ya wachezaji watatu waliovuka umri kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo.
Kutokana na kipaji chake kikubwa na umaarufu wake, dhahiri anastahili nafasi. Bado Mexico ina washambuliaji wawili ambao walifanya vizuri wakati wa kuwania kufuzu Olimpiki ambao ni Alan Pulido na Marco Fabian.
Pulido, ambaye alifunga mabao matano katika mechi tano za kufuzu Olimpiki, anatarajiwa kung’ara kwenye michuano hiyo.
Fabian, ambaye alifunga mabao matano katika kuwania kufuzu, naye anapewa nafasi ya kung’ara.
0 comments:
Post a Comment