Drogba ambaye chini ya AVB alionekana kafilisika kisoka |
ANDRE Villas-Boas ni lazima atakuwa ameketi
huko aliko na kukuna kichwa chake kutokana na kile kinachoendelea kutokea Chelsea kwa sasa.
Ni lazima atakuwa anashangwa na kile
kinachoendelea kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge .
Mreno huyo, AVB alitua Chelsea na kuanzisha vitu vipya kabisa kwenye
kikosi hicho vya ndani na nje ya uwanja na kufanya filosofi iliyoonekana kuwa
mtihani mgumu kueleweka na nyota wake.
Aliwaweka kando wachezaji wazee,
akawaingiza vijana na kutaka kucheza kwa nidhamu kubwa na soka la kisasa – huku
akilenga kwenye mambo yajayo. Unafahamu nini kilimtokea?
Kuondoka kwake kumefungua njia kwa
aliyekuwa msaidizi wake, Roberto Di Matteo kushika usukani. Muitaliano huyo
anatambua namna ya kwenda na kikosi kama hicho cha Chelsea kilichoegemea zaidi kwa wachezaji
wenye umri mkubwa.
Di Matteo akatoa uhuru kwa wachezaji wake
na kuacha kuwabana kwa mambo ya nje ya uwanja. Jambo hilo
limeifanya timu hiyo kurudi kwenye makali yake na kuwa Chelsea tishio.
Matokeo ya hilo . Chelsea
sasa imekuwa ni moja ya timu hatari zaidi England na kwenye mikikimikiki ya
Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Kama timu hiyo ingeendelea kubaki chini ya AVB
ni wazi hali ingekuwa mbaya zaidi kutokana na filosofi za Mreno huyo kutaka
kuwaendeesha wachezaji wenye umri mkubwa kama
Frank Lampard kama vile wangali watoto.
Huwezi kumfundisha mambo ya kufanya Lampard
anapokuwa kwenye shughuli zake za nje ya uwanja au kumbana kama utakavyofanya
kwa kinda kama Daniel Sturridge, ambaye
utahitaji awe na nidhamu ili kulinda kipaji chake kichanga.
Tangu AVB alipoondoka na ‘vibabu’ vya Chelsea vimepata uhuru wao
– vimeweza kuwa tishio na sasa zimetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa barani na
Kombe la FA.
AVB aliwabana wachezaji hao – kitu ambacho
awali alipata nguvu kubwa kutoka kwa bosi wake, Abramovich – kabla ya mambo
kumgeukia na kuonyeshwa njia ya kutokea.
RDM amechukua mikoba, amekikusanya kikosi
hicho na kukirudisha pamoja kama kundi na hivyo kurejea kwenye kasi yao ya ushindi na
ukichanganya na bahati ya Muitaliano huyo, basi mafanikio hayo yanamfanya aonekane
‘genius’.
Ni hadithi inayofurahisha. Wakati AVB alipokwenda
na kikosi chake cha Chelsea
kumenyana na QPR Loftus Road
– Oktoba mwaka jana, Jose Bosingwa na Didier Drogba walitolewa kwa kadi
nyekundu, kadi saba za njano na Blues ilipokea mkong’oto wa 1-0.
Kilikuwa ni kipindi ambacho hali ilikuwa
mbaya zaidi ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo kwenye klabu hilo . Kipindi ambacho Fernando Torres alishindwa
kutikisa nyavu na hivyo kuonekana kama hawezi
kuvaa buti za Drogba katika kuisaidia timu hiyo.
Na sasa miezi sita baadaye, unajua nini
kimetokea? Maajabu mawili ndani ya wiki moja. Kwanza
tukio lile la Nou Camp na sasa hili ambalo pengine ni kubwa zaidi, la kumfanya Torres
kurejea kwenye kasi yake ya kufumua nyavu.
Mhispania huyo alifunga ‘hat-trick’ yake ya
kwanza tangu alipojiunga na timu hiyo na hivyo kuongeza kwa mara mbili mabao
yake kwenye ligi.
Na hapo Chelsea ikapata ushindi wake mkubwa kabisa
kwa msimu huu, wakati walipoikung’uta QPR 6-1.
Frank Lampard alicheza kwa kiwango kikubwa,
Ashley Cole alicheza kama beki bora kabisa barani Ulaya na Bosingwa, ambaye
alishindwa kuingia kwenye kikosi hicho – anacheza kama
beki wa kizamani wa kati.
Hiyo ni wazi kabisa kwamba baadhi ya
wachezaji wakongwe na wenye uzoefu katika kikosi hicho hawakuwa tayari kucheza
dhidi ya AVB.
Wakati Chelsea inafunga bao lake la nne
juzi, mvua ilinyesha na muda mfupi baadaye jua lilitoka jambo lililodhihirisha
wazi kwamba hata Mungu yupo upande wa Di Matteo.
Kutokana na yote hayo, kwanini Muitaliano
huyo asitajwe kuwa kocha wa kudumu kwenye kikosi hicho?
Kikosi hicho kwa sasa kipo kwenye fainali
mbili. Je, nini hatima ya RDM kama ataweza
kunyakua mataji yote mawili?
Kwa matokeo yoyote yatakayotokea, Chelsea kwa sasa inafurahia nyakati nzuri kabisa
zilizowahi kutokea kwenye kikosi chao ni wazi mafanikio haya ni kama yanamwacha mtupu AVB – ambaye alishindwa kuhamishia
makali yake ya FC Porto kwenye klabu hiyo ya ‘darajani’.
0 comments:
Post a Comment