Chelsea imeonyesha kiwango usiku huu na kufuzu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kucheza 10, lakini wamelazimisha sare ya 2-2 na wenyeji Barcelona katika bonge la marudiano la Nusu Fainali kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Sergio Busquets alifunga bao la mapema dakika ya 35, dakika chache kabla ya Nahodha wa Chelsea, John Terry kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu Alexis Sanchez nyuma ya mpira.
Andres Iniesta akafunga la pili ambalo lilionekana kama la ushindi, lakini Ramires akaifungia Chelsea kabla ya mapumziko na kabla Lionel Messi hajakosa penalti kipindi cha pili, baada ya Cesc Fabregas kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Messi tena akakosa bao la wazi baada ya kupiga shuti dhaifu na Fernando Torres aliyetokea benchi akafunga bao la pili kwa Chelsea dakika ya mwisho na kuivusha Roberto Di Matteo’ katika fainali ya michuano hiyo itakayopigwa mjini Munich.
0 comments:
Post a Comment