Cheka kuliaakisaini mbela ya promota Kaike Siraju katikati |
BINGWA wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC,
Francis Cheka wa Morogoro amesaini
mkataba wa kupigana na bingwa wa Kick
Boxing. Japhet Kaseba katika uzito wa Middle
utakaofanyika Julai 7, mwaka huu mjini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema
anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika
mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi
wanamtaka kupigana na yeye.
“Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na
mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila
anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi
yangu,” alisema Cheka.
“Kaseba nilimpiga kwa KO Oktoba 3, mwaka 2009, anataka tena
wembe kwa ngumi ni sehemu ya maisha
yangu, siwezi kukataa na mimi ndio napata riziki yangu humu, hivyo
nitahakikisha anayekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma, nitaanza na Mada
Maugo Aprili 28 na huyo namuweka kama kiporo
Naye Promota wa mpambano huo, Kaike Siraju amesema mbali na
mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali
ambazo mtatangaziwa baadae.
0 comments:
Post a Comment